1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabila asema uchaguzi wa Congo utafanyika

19 Julai 2018

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, amehutubia bunge ikiwa ni chini ya wiki moja kabla ya wagombea hawajaanza kujisajili kwa ajili ya uchaguzi wa rais ulioahirishwa.

https://p.dw.com/p/31kq7
Rais Joseph Kabila
Picha: YouTube/CleboaPointCom News

M M T/ Interview Milongo - MP3-Stereo

Nchi hiyo kubwa barani Afrika imesubiri kusikia kama Kabila atagombea katika uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu ukiwa umepangwa kufanyika mwezi Desemba licha ya muhula wake kikatiba kumalizika mwaka 2016. Rais Kabila amekataa kutangaza hadharani iwapo atagombea muhula mwingine madarakani au la, na wagombea urais wanatarajiwa kusajiliwa kati ya tarehe 25 mwezi huu hadi tarehe mosi Agosti.

Wiki iliyopita katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema alikubali kuahirisha ziara yake nchini Congo ili kumruhusu Kabila kutangaza maamuzi mazito. Kabila ambaye alichukua madaraka kutoka kwa baba yake aliyeuawa mwaka wa 2001, alimaliza muhula wake kisheria mwaka 2016 lakini vifungu vya katiba vilimruhusu kusalia madarakani hadi mrithi wake atakapopatikana.