1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Raia wauwawa tena katika shambulio la majeshi ya Marekani.

1 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmu

Maafisa nchini Afghanistan wamesema kuwa shambulio la anga lililofanywa na majeshi ya washirika wa Marekani ambalo lilisababisha vifo vya waasi 35 wa taliban siku ya Ijumaa pia limesababisha vifo kadha vya raia.

Afisa mmoja nchini humo amedai kuwa kiasi cha raia 65 wameuwawa katika mapigano yaliyotokea katika wilaya ya Girishk kusini mwa jimbo la Helmand.

Jeshi hilo linaloongozwa na Marekani limesema , ndege za majeshi ya washirika pamoja na jeshi la kimataifa linalosaidia kuweka usalama ziliitwa katika eneo hilo baada ya majeshi hayo kushambuliwa na wapiganaji.

Akizuru mjini Kabul , waziri wa mambo ya kigeni wa Australia Alexander Downer amesema majeshi ya NATO yamefanya kila jitihada kuepuka vifo vya raia. Amelaumu mauaji hayo kuwa yanatokana na mbinu za wapiganaji wa Taliban.