1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Taliban yaanza mazungumzo na Korea Kusini

11 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaI

Nchini Afghanistan wawakilishi wa kundi la Taliban wameanza mazungumzo ya ana kwa ana na ujumbe wa Korea Kusini juu ya kuachilliwa kwa mateka 21.

Mkutano huo ni wa kwanza kufanyika ana kwa ana tokea Wakorea Kusini watekwe nyara na wanamgambo wa Taliban mwezi uliopita.Taliban imesema imehakikishiwa usalama na serikali ya Afghanistan kukutana na ujumbe huo katika Ofisi ya Chama cha Msalaba Mwekundu huko Ghazni karibu na mahala walikotekwa Wakorea hao.

Wajumbe kadhaa wa Kamati ya Kimataifa ya chama cha Msalaba Mwekundu inaonekana kwamba pia wanahudhuria mazungumzo hayo.

Wanamgambo wa Taliban wanataka serikali ya Afghanistan iwaachilie waasi wenzao walioko magerezani kwa kubadilishana na wafanyakazi hao wa misaada wa Korea Kusini.

Wakati huo huo imefahamika kwamba baada ya kukwepa kikao cha ufunguzi cha pamoja cha siku tatu kati ya Afghanistan na Pakistan cha amani katika baraza la jirga kinachofanyika nchini Afghanistan kwa nia ya kukomesha harakati za Taliban na kuleta amani nchini humo Rais Pervez Musharraf wa Pakistan leo atahuhudhuria ufungaji wa kikao hicho.

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amempigia simu Musharraf jana jioni na kumualika kuhudhuria kikao hicho cha pamoja ambapo amekubali kimsingi kuhutubia ufungaji wa kikao hicho.