1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya Rais Bongo wa Gabon yatupwa nje

21 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cerd

PARIS:

Mahakama moja mjini Paris, imetupilia mbali kesi ya rais Omar Bongo wa Gabon dhidi ya mshauri wake wa zamani na pia aliekuwa afisa wa kampuni ya mafuta ya kifaransa –Elf. Inasemekana kuwa rais Bongo aliwasilisha kesi hiyo akitaka mpambe wake wa zamani-Andre Tarallo,akabidhi kwa raia huyo umilikaji wa majengo mawili -moja likiwa Corsica na lingine Paris pamoja na pesa taslimu za mamiliioni ya dola.

Tarallo,aliewahi kuwa afisa wa juu aliehusika na mashauri ya kiafrika katika kampuni ya mafuta ya ELF,aliwahi, wakati mmoja, kuwa mshauri wa Bongo katika miaka ya 1990.Na wakati fulani katika kesi nyingine ya ufisadi, alikiri kuwa alipokea pesa kadhaa kwa niaba ya rais.

Mahakama imeamua kuwa Tarallo, aliehukumiwa kwa ubadhilifu wa pesa zinazisemwa katika korti nyingine Machi mwa wa 2005 na kwa hivyo Gabon haiwezi kuendelea na kesi ambayo imesha amuliwa na mahakama ya makosa ya jinai.