1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Bunge la Urusi lakosoa amri ya rais wa Ukraine

6 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCC4

Bunge la Urusi limekosoa amri ya rais Viktor Yuschenko wa Ukraine ya kuvunja bunge la nchi hiyo na kuitisha uchaguzi wa mapema.

Duma, bunge la Urusi limepitisha azimio kuwa amri hiyo ya rais Yuschenko imeenda kinyume cha sheria.

Spika wa bunge la Urusi Boris Gryslow ameeleza wasiwasi juu ya matukio nchini Ukraine.

Rais Yuschenko ameonya kuwa mfanyakazi yoyote wa serikali atakae puuza amri hiyo atachukuliwa hatua kali.

Waziri mkuu wa Ukraine Viktor Yanukovich ameliambia baraza lake la mawaziri lisijitayarishe kwa uchaguzi hadi mahakama ya katiba itakapo toa uamuzi juu ya amri ya rais Yuschenko.