1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim Jong Un: Jeshi liziangamize Marekani na Korea Kusini

Tatu Karema
1 Januari 2024

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameliamuru jeshi lake "kuziangamiza kabisa" Marekani na Korea Kusini ikiwa taifa hilo litachokozwa.

https://p.dw.com/p/4alxY
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: KCNA/REUTERS

Shirika la habari la serikali KCNA limesema Kim ameapa kuimarisha ulinzi wa taifa hilo kukabiliana na kile alichokiita mzozo mkubwa unaoongozwa na Marekani ambayo hayajawahi kushuhudiwa.

Katika mkutano wa Jumapili na maafisa wakuu wa jeshi, Kim alisema ni muhimu kujiandaa na ''silaha yake ya thamani' ili kulinda usalama wa taifa, akimaanisha mpango wa silaha za nyuklia wa nchi yake.

Soma pia: Kim Jong Un asifu mafanikio ya Korea Kaskazini mwaka 2023

KCNA imeendelea kuripoti kuwa Kim pia alitaja kuhusu hatua za makabiliano ya kijeshi ya Marekani na vikosi vingine vya uadui.

Katika mkutano mkuu wa siku tano wa chama tawala wiki iliyopita, Kim alisema kuwa mwaka huu, atazindua satelaiti tatu zaidi za ujasusi wa kijeshi, kutengeneza silaha zaidi za nyuklia na ndege zisizo na rubani katika kile waangalizi wanasema ni jaribio la kuongeza uwezo wake katika diplomasia ya baadaye na Marekani.