1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongamano la makanisa ya Kiinjili laendelea Dresden Ujerumani

2 Juni 2011

Masuala ya imani, maadili na mchango wa kanisa katika jamii ni mambo yanayojadiliwa kwenye kongamano hilo.

https://p.dw.com/p/11T8y
Washiriki wa kongamano la DresdenPicha: dapd

Kongamano la 33 la makanisa ya Kiinjili limeingia siku yake ya pili leo (02.06.2011)katika mji wa Dresden ulio mkoani Saxony hapa Ujerumani. Mkutano huo utakaohitimishwa tarehe 5 mwezi huu unawaleta pamoja waumini wa makanisa ya Kiinjili kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni. Kauli mbiu ya kongamano hilo ni ,"Unachokithamini, ndicho cha tunu".

Mada muhimu zinazojadiliwa ni pamoja na masuala ya imani, maadili na mchango wa kanisa katika jamii ukiyazingatia masuala ya demokrasia na usawa. Ili kupata picha halisi ya mambo yanavyoendelea Thelma Mwadzaya alizungumza na Veronica Natalis, mshiriki kutoka Shinyanga, Tanzania anayehudhuria kongamano hilo la Dresden.

Mwandishi: Thelma Mwadzaya

Mhariri: Josephat Charo