1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Huenda likawa kombora la kushambulia bara moja hadi jengine.

Faiz Musa18 Aprili 2019

Korea ya Kazkazini imesema imefanya jaribio la silaha nyengine mpya na wakati huo huo kuitaka Marekani kumuondoa waziri wake wa mambo ya nje Mike Pompeo katika mazungumzo ya baadaye ya Nuklia.

https://p.dw.com/p/3H2RY
Kim Jong Un und Mike Pompeo
Picha: picture alliance/AP Photo

Jaribio hilo ambalo halikuonekana kama limekiuka masafa yaliyopigwa marufuku ya makombora ya nuklia imeliruhusu taifa hilo kuonyesha kwamba linaendelea na kutengeza silaha za nuklia na vile vile kuwahakikishia wakuu wa jeshi la nchini humo kuwepo kwa ishara za udhaifu wa kidipolomasia na Marekani.

Mchambuzi kutoka eneo la Korea Kazkazini alisema taarifa zilizoko katika vyombo vya habari katika taifa hilo zinatoa ishara ya kwamba silaha iliyojaribiwa ni kombora jipya ambalo linaweza kushambulia bara moja hadi jengine.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa idara ya mambo ya Marekani katika wizara ya masuala ya kigeni ya Korea Kazkazini, ilimshutumu Pompeo kwa kudharua matamshi muhimu ya rais Kim Jong Un na vile vile kupuuza matakwa ya Korea Kazkazini ya kutaka mazungumzo ya Nuklia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Nordkorea Raketentest
Kombora kutoka baharini nchini Korea Kazkazini (2015), rais Kim alikuwepo kushuhudia jaribio hiloPicha: picture-alliance/dpa/KCNA

Taarifa hiyo ilimtaja Pompeo kama mtu wa kubuni mambo wakati katika hotuba yake siku ya Jumatatu alipopinga kauli ya Kim ya makataa ya mazungumzo ya Nuklia aliposema angependa mpango huo kukamilika hivi karibuni.

Korea Kazkazini inasema kuendelea kwa Pompeo kuwa katika mazungumzo hayo ni kuhakikisha kwamba mazungumzo hayo yanakorogeka hivyo basi kuitaka Marekani kumbadilisha na mtu mwengie aliye makini zaidi na mweledi wa mawasiliano.

Rais Kim kusafiri kwenda Urusi

Wakati huo huo Urusi ilisema rais wa Korea kazkazini Kim Jong Un atatembela taifa la Urusi mwishoni mwa mwezi huu wa nne. Taarifa fupi kutoka ikulu ya Urusi imethibitisha kwamba Rais Vladimir Putin amemualika Kim.

Ziara ya Kim Urusi itampa Putin nafasi ya kuwa mpatanishi katika mvutano huo wa muda mrefu wa silaha za Nuklia hivyo basi kuiinua hadhi ya Urusi katika masuala ya kikanda.

Russland Präsident Putin besucht Südrussland
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: picture-alliance/TASS/M. Klimentyev

Vile vile Rais Putin atazuru China mwishoni mwa mwezi huu ambapo anatarajiwa kukutana na Kim katika mji wa bandari wa Vladivostok karibu na mpaka wa Korea Kazkazini.

Baadhi ya wachambuzi wanasema kitendo cha Korea Kazkazini kufanya majaribio ya makombora ya nuklia ni njia ya kuilazimisha Marekani kuacha msimamo wake mgumu na kukubaliana na matakwa ya Koerea kazkazini ya kuwaondolea vikwazo vya kimataifa.

Wiki jana Kim alisema yuko tarayi kwa mkutano wa tatu na rais Donald Trump ila akaweka makataa ya mwisho wa mwaka huu kwa Marekani kutoa matakwa ya kukubalika juu ya mpango huo.

(APE)