1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

India na Pakistan kwanini zinazozana juu ya mkataba wa IWT?

Saumu Mwasimba
16 Februari 2023

India inashinikiza mkataba wa kihistoria kuhusu matumizi ya maji ya mto Indus na vyanzo vyake vitano, uliosainiwa kati ya nchi hiyo ya jirani yake Pakistan mnamo mwaka 1960 ujadiliwe upya.

https://p.dw.com/p/4NY5h
Indien Kaschmir Fluss Chenab
Picha: Mohammad Abu Bakar/Pacific Press/IMAGO

Waziri mkuu wa nchi hiyo Narendra Modi anataka mkataba huo ujadiliwe upya lakini wengi nchini humo hivi sasa wanaitolea mwito serikali ijiondowe kabisa kwenye mkataba huo.

Kuongezeka mvutano kati yaIndia na Pakistan kuliichochea Pakistan kulipeleka suala  hilo mbele ya mahakama ya kimataifa ya usuluhishi mjini The Hague.

Hata hivyo maafisa wa India walikataa kuhudhuria kikao cha kwanza kilichofanyika mwishoni mwa mwezi Januari na kuwaacha wawakilishi wakijikuta peke yao mbele ya maafisa wa mahakama hiyo.

Msimamo wa India ni kwamba mahakama ya usuluhishi ya The Hague, PCA haina uwezo wa kuyaangalia maswala yanayohusika kwenye mkataba huo wa matumizi ya maji ya mto Indu IWT na kwamba panahitajika njia nyingine mbadala itakayosimamiwa na wataalamu.

Mahakama ya usuluhishi mjini The hague imeshaonesha kwamba iko tayari kutoa maamuzi kuhusiana na uwezo wake kwenye suala hilo mnamo mwezi Juni mwaka huu.

Soma pia:Ujerumani na India kushirikiana kulinda mazingira

Kimsingi kwa mujibu wa mkataba wa IWT India ina mamlaka ya kusimamia mito mitatu upande wa Mashariki ambayo ni Beas,Ravi na Sutlej wakati Pakistan nayo ikiwa na mamlaka ya kusimamia mito mitatu mengine iliyoko upanda wa Magharibi ya Jhelum,Chenab na Indus ambayo inapeleka maji mpaka sehemu ya India ya Kashmir na kuingia Pakistan.

India inaweza kutumia asilimia 20 ya maji ya mito hiyo mitatu ya Magharibi kwa matumizi yake ya umwagiliaji,usafiri na uzalishaji umeme.

Matakwa ya mkataba wa IWT

Mkataba huo wa mwaka 1960 pia uliunda tume ya kudumu ambayo inawawakilishi wa pande zote mbili wanaofanya kazi ya utekelezaji wa kufikiamalengo ya kugawana maji ya mto Indus.

Indien Kaschmir Fluss Jhelum
Mto Jhelum Kashmir IndiaPicha: ingimage/Wirestock/IMAGO

 Utaratibu huo umefanikiwa kuwepo kwa miongo na kunusurika kwenye uhasama na mivutano ya kipindi chote hicho na hata vita kati ya nchi hizo mbili.

Soma pia:Ujerumani na India zimeashiria kuwa tayari kutanua ushirikiano

Lakini hivi sasa mivutano imeongezeka kwa mara nyingine na wataalamu wanatahadharisha kwamba itakuwa vigumu  kuingia kwenye majadiliano mapya kuhusu mkataba huo ikiwa serikali ya India itachukuwa uwamuzi wa kivyake kujiondowa kwenye mkataba.

Mchambuzi wa kisiasa Reyaz Ahmad ameiambia Dw kwamba kuna ukosefu mkubwa wa hali ya kuaminiana kati ya pande mbili.

Ameongeza kwamba ikiwa tathmini ya wataalamu juu ya mkataba huo,inawezekana,katika wakati ambapo kuna maswala makubwa ya msingi kama mabadiliko ya tabia nchi.

Jicho la kidiplomasia katika mzozo

Wachambuzi wa kisiasa wanaamini ikiwa India itachukuwa uwamuzi wa peke yake wa kujiondowa kwenye mkataba huo basi hapana shaka huenda ukachochea chuki na upinzani kutoka Pakistan.

Lakini chuki na upinzani inaweza pia kuwa ni mwanzo tu,na ikiwa India itaamuwa kuyazuia maji ya mito mitatu ya upande wa Magharibi inayotumiwa na Pakistan  basi itasababisha athari katika shughuli za kilimo za Pakistan kwa asilimia kiasi 62.

Mchambuzi wa kisiasa Ahmad anasema maafisa wa pande zote mbili wanapaswa kutazama haki na kuchukua hatua zinazostahiki.

 Anahoji kwamba mkataba huo umehimili mitihani mingi tangu ulipotiwa saini miongo sita iliyopita ukishuhudia vita mara tatu na kwahivyo sio busara kuvurugwa.

Soma pia:Modi amwambia Putin huu si wakati wa vita

Na mkataba huo kwa jicho la mchambuzi huyo ni mfano unaoonesha diplomasia linapohusika suala la maji.

Mapango yawahifadhi wasio na makaazi Pakistan