1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London.Uingereza yadhamiria kulipa mamlaka ya usalama jeshi la Iraq.

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCq7

Waziri wa kigeni wa Uingereza Margaret Beckett amesema, Uingereza itakabidhi dhamana ya masuala ya kiusalama kusini mwa Iraq katika mji wa Basra kwa mamlaka ya Iraq katika msimu ujao wa kiangazi.

Kwa hivi sasa kuna kiasi cha wanajeshi wa Uingereza 7,000 wanaolinda amani nchini humo.

Akielezea mpango huo wa kuvipa nafasi vikosi vya Iraq kuchukua dhamana Waziri Becket amesema.

“Utaratibu wa kuwajibika vikosi vya usalama vya Iraq katika masuala ya ulinzi, umeshaingia njiani. Na waziri mkuu Maliki amepania kuuendeleza na sie pia tumepania kumsaidia na kuhakikisha anafanikiwa kikamilifu. Tunataraji Najaf utakuwa mkoa mwengine kuwa chini ya Ulinzi wa Wa-Iraq kuanzia mwezi ujao wa December“.

Wakati huo huo ripoti ya Umoja wa Mataifa imedai kuwa idadi ya raia waliouwawa nchini Iraq katika mwezi wa October iliongezeka zaidi kuliko miezi yote iliyotangulia.