1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano dhidi ya mkutano wa G20 yaanza Ujerumani

3 Julai 2017

Maelfu ya watu waandamana huko Hamburg Jumapili (02.07.2017) kupinga mkutano wa kilele ujao wa G20 wa nchi zilizostawi kiuchumi na zile zinazoinukia kiuchumi ambapo Rais Donal Trump wa Marekani anatarajiwa kuhudhuria.

https://p.dw.com/p/2fn9p
Protestwelle gegen den G20 Gipfel
Picha: picture-alliance/dpa/M. Scholz

Maelfu ya watu waandamana huko Hamburg Jumapili (02.07.2017) kupinga mkutano wa kilele ujao wa kundi la G20 la nchi zilizostawi kiuchumi na zile zinazoinukia kiuchumi ambapo Rais Donal Trump wa Marekani anatarajiwa kuhudhuria.

Wakati kukiwa na kiwingu hicho cha kupinga utandawazi Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema Jumapili viongozi itabidi wazingatie suala la ukuaji wa kiuchumi endelevu na shirikishi badala ya kuzingatia ustawi wa mataifa yao tu.

Katika hotuba ya mtandaoni Kansela huyo wa Ujerumani amesema mkutano wa kilele wa kundi la mataifa 20 yalioendelea  na kuinukia kiuchumi wa mwaka huu utaangalia masuala yanayopiganiwa na waandamanaji kama vile kutawanya utajiri na matumizi ya rasilmali sambamba na masuala yanayohusiana nayo kama vile mabadiliko ya tabia nchi,masoko huru, ulindaji wa walaji na kushikilia viwango vya kijamii.

Maandamano 30 kufanyika kabla ya mkutano wa kilele wa G20

Deutschland Hamburg - G20 Proteste
Maelfu wakiandamana Hamburg dhidi ya mkutano wa kilele wa G20. unaoanza wiki ijayo.Picha: Getty Images/AFP/J. Macdougall

Maelfu ya waandamanaji waliandamana huko Hamburg Jumapili kupinga mkutano huo wa kilele uliopangwa kufanyika tarehe saba hadi nane ambapo polisi 21,000 kutoka kila mahala Ujerumani watamwagwa kuilinda mikutano ya mataifa makubwa ishirini yalioendelea kiuchumi na yanayoinukia kiuchumi duniani.

Hamburg ambako mwenyeji wa mkutano huo wa kilele wa G20 Kansela Angela Merkel ndiko alikozaliwa ni mji mchangamfu na pia ni ngome ya makundi ya sera kali za mrengo wa kushoto yenye kupinga serikali.

Takriban maandamano 30 yamepangwa kufanyika kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa kilele ambapo waandalizi wa maandamano hayo wanataraji jumla ya watu 100,000 watajitokeza kwenye maandamano hayo.

Uwezekano wa kuzuka hujuma na uharibifu

Deutschland Hamburg - G20 Proteste
Waandamanaji wakiwa na masanamu wanayoyafananisha na viongozi wa nchi za G20.Picha: Reuters/F. Bimmer

Waziri wa mambo ya ndani Thomas de Maziere katika toleo la Jumapili la gazeti la Ujerumani la Bild ameonya kwamba ghasia "zinapaswa kudhibitiwa kwenye kiini ."Amesema "Uhuru wa kukusanyika unakuwa tu na maana kwa maandamano ya amani."

Merkel amesema mkutano huo wa kilele utakuwa sio tu kuhusu ukuaji wa kiuchumi bali ukuaji wa uchumi endelevu.Amesema "inabidi kila mtu afaidike ni masuala hayo ambayo yanazunguka: suala vipi tutafanikisha ukuaji wa uchuni shirikishi au endelevu?"

Merkel anayewania muhula wa nne madarakani katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Septemba 24 ameyaelzea masuala kayo kama vile: Tunafanya nini na rasilmali zetu? Taratibu ni zipi katika kutawanya utajiri? Watu wangapi wanashiriki?Na nchi ngapi zinaweza kufaidika na hayo?"

Bila ya kutaja maandamano ambayo yanawatia wasi wasi vikosi vya usalama nchini Ujerumani kuhusu uwezekano wa kuzuka kwa vitendo vya hujuma wiki hii katika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Merkel amesema masuala ambayo sio ya jadi imelazimika kuyaingiza katika agenda ya mkutano huo wa G20.

Onyo kali

Deutschland Hamburg - Demonstration wegen Durchsuchungen
Polisi wakiijiandaa kukabiliana na waandamanji Hamburg.Picha: picture-alliance/dpa/B. Marks

Merkel amesema "iwapo watajaribu tu kuendelea na mkutao wao kama walivyofanya huko nyuma hatua za mendeleo duniani kote hazitokuwa endelevu na shirikishi."  na kwamba "Tunahitaji makubaliano ya kulinda tabia nchi,masoko huru na kuboresha makubaliano ya kibishara ambayo kwayo suala la kumlinda mlaji, viwango vya kijamii na mazingira vitakuwa vinaendelezwa."

Katika hotuba bungeni wiki iliopita Merkel ameahidi kupigania biashara huru na kushinikiza juhudi za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi wakati wa mkutano wa kilele wa G20 kwa kupingana na sera za Rais Doland Trump wa Marekani za "Marekani Kwanza."

Serikali ya Ujerumani ina wasi wasi wa kuzuka ghasia huko Hamburg kwa makabiliano na polisi yatakayojumuisha uharibifu wa mali.Jumla ya polisi 15,000 watawekwa kuulinda mkutano huo wa kilele ikiwa ni ziada ya polisi 3,800 watakaosimamia usalama viwanja vya ndege na vituo vya treni.

Mwandishi : Mohamed Dahman/Reuters/AFP

Mhariri : Bruce Amani