1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSerbia

Maelfu waandamana Serbia kupinga matokeo ya uchaguzi

30 Desemba 2023

Maelfu ya watu wameandamana Jumamosi katika mji mkuu wa Serbia, Belgrade, huku wakipiga zogo kwa kumshutumu rais wa nchi hiyo Aleksandar Vucic kuendesha udanganyifu wakati wa uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa.

https://p.dw.com/p/4ajJF
Belgrad, Serbien 2023 Studentenproteste gegen angeblichen Wahlbetrug in Belgrad
Waandamani mjini Belgrade nchini Serbia wakipinga matokeo ya uchaguzi: 29.12.2023Picha: Andrej Isakovic/AFP

Kwa karibu wiki mbili sasa, Serbia imekuwa ikishuhudia maandamano makubwa ya kupinga kasoro zilizoshuhudiwa wakati wa uchaguzi huo uliofanyika Desemba 17 mwaka huu, kasoro zilizoainishwa pia na waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi.

Chama tawala cha Serbian Progressive Party kilitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo lakini muungano mkuu wa upinzani wa Serbia Against Violence, unadai kuwepo wizi wa kura na wameomba kuwepo tume ya kuchunguza kasoro hizo na ikihitajika uchaguzi huo urudiwe.