1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Mashirika ya haki za binadamu yakosoa kamatakamata Niger

26 Oktoba 2023

Mashirika ya kutetea haki za binadamu Human Rights Watch na Amnesty International yamesema kwamba mamlaka za Niger zimewakamata kiholela makumi ya maafisa wa serikali iliyoondolewa madarakani.

https://p.dw.com/p/4Y4IC
	
Niger Niamey | Abdourahamane Tiani
Picha: Télé Sahel/AFP

Kukandamiza vyombo vya habari vinavyoikosoa serikali na wapinzani wasiotumia nguvu tangu yalipofanyika mapinduzi ya kijeshi Julai 26, 2023. 

Mashirika hayo yamesema mamlaka zinapaswa kuwaachilia huru mara moja wale wanaoshikiliwa kwa tuhuma zinazochochewa kisiasa na kuhakikisha kunatafutwa utaratibu unaofaa .

Soma pia: Utawala wa kijeshi kumfungulia mashtaka ya uhaini Bazoum

Kulingana na Ilaria Allegrozzi, mtafiti mkuu wa shirika la Human Rights Watch,tawi la Sahel, hatua ya jeshi kuwakamata watu kiholela na kukiuka haki ya uhuru wa kujieleza kunaiweka Niger kwenye njia hatari linapokuja suala la haki za binadamu. Na ameitolea mwito mamlaka kusitisha kamatakamata za kiholela, kuzingatia haki za binadamu, na kuruhusu vyombo vya habari kuwa huru.

Mnamo Julai 26, Jenerali Abdourahmane Tiani na maafisa wengine wa jeshi la Niger wa Baraza la Kitaifa la Ulinzi wa Nchi walipindua serikali ya Rais Mohamed Bazoum.

Kunyamazisha ukosoaji

Paris Protest Putsch Niger Mohamed Bazoum Plakat
Bango lenye picha ya Bazoum, lililo na ujumbe wa kumuunga mkono.Picha: Sophie Garcia/AP Photo/picture alliance

Tangu mapinduzi hayo Bazoum, mke wake na mwanawe wamezuiliwa katika ikulu ya rais huko Niamey, na maafisa wengine wamekamatwa. Jeshi pia limewatishia, limewanyanyasa, na kuwakamata kiholela waandishi wa habari, vijana, na wanaochukuliwa kuwa wapinzani wa kisiasa, pamoja na wakosoaji wengine wanaotoa maoni yao.

Soma pia: Utawala wa kijeshi Niger wamzuia Mwanadiplomasia wa Marekani kumuona Bazoum

Aidha  mamlaka imewakamata bila ya kuzingatia sheria maafisa kadhaa wa serikali iliyoondolewa madarakani, akiwemo Sani Mahamadou Issoufou, aliyekuwa waziri anayesimamia mafuta ya petroli; Hamadou Adamou Souley, waziri wa zamani wa mambo ya ndani; Kalla Moutari, aliyekuwa waziri wa ulinzi; na Ahmad Jidoud, waziri wa zamani wa fedha.

Mnamo Septemba, mamlaka ya Nigeriliwahamisha hadi kwenye magereza ya Filingué Say, Kollo katika eneo la Tillaberi, na Niamey, na kuwafungulia mashtaka ya "kutishia usalama wa taifa" mbele ya mahakama ya kijeshi, licha ya wao kuwa raia, kinyume na utaratibu uliowekwa. Mashirika ya Amnesty International na Human Rights Watch yanaitazama hatua ya  kukamtwa kwa maafisa hao kama iliyochochewa  kisiasa.

Human Rights Watch imeelezea wasiwasi wake  juu ya hali ya Bazoum na ustawi wa familia yake. Bazoum aliwasilisha ombi katika Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi-ECOWAS huko Abuja, Nigeria, akitaja ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi yake na familia yake wakati wakiwa kizuizini. Pia alitaka kurudishwa madarakani mara moja kama rais wa Niger.

Waandishi wa habari wa kitaifa na kimataifa wamekuwa wakipewa vitisho, kunyanyaswa kwa maneno mtandaoni, na kushambuliwa.

Serikali ya Niger, imezinyamazisha sauti zinazoikosoa na mnamo Agosti 22, 2023, kiongozi wa jeshi Abdourahmane Tiani, alitangaza amri bila ya kutowa ufafanuzi ya kuwaondoa wasomi sita ambao pia walikuwa maafisa wa serikali na siku moja kabla ya hapo wale waliondolewa walikuwa wamesaini pamoja na wasomi wengine tamko la kujitenga  na taarifa iliyotolewa Agosti mosi na chama cha waalimu na watafiti iliyoiunga mkono baraza la utawala la Kijeshi.

 

//https://www.hrw.org/news/2023/10/26/niger-authorities-putting-rights-risk