1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matatu Kenya zawainua maDJ chipukizi

8 Desemba 2015

Nchini Kenya utamaduni wa kuendesha matatu huku muziki unachezwa umejikita. Hiyo imetoa fursa kwa maDJ chipukizi kupata fursa ya kukuza vipaji vyao na kujipatia riziki

https://p.dw.com/p/1HJ6T
Reportage Africa on the Move Kenia DJ Brownskin Matatu Fahrer
Picha: Julia Mielke

Matatu Kenya zawainua maDJ chipukizi

Mji mkuu wa Kenya-Nairobi ni mji wa shughuli nyingi wenye wakaazi takriban milioni nne na unajulikana kwa kuwa na msongamano wa magari. Matatu, mojawapo ya magari ya usafiri wa umma yanatoa taswira ya mitaa ya mji huo hasa kuelekea katika sehemu ya biashara ya jiji.

Ushindani kati ya madereva wa basi ni mkubwa. Kwa wateja wengi vijana, muziki mzuri katika matatu hizo ni kitu kinachowavutia wanapokuwa wamekwama katika trafiki. Kwa hivyo utamaduni wa kuendesha magari na kusikiliza muziki umejijenga. Hilo limesababisha mfuatano wa utengenezaji wa muziki, wachangaji muziki au madijei wanaochanganya miziki ya kisasa inayovuma na kuuza kwa matoaji wadogo na wakubwa ambao wanawauzia madereva wa matatu.

Na ma-Dj wachanga wanapata fursa ya kujulikana na umma na hata kuanzisha tasnia ya udijei. Imekuwa biashara iliyoshamiri. Vijana wengi zaidi wanataka kuwa ma-DJ na kuna vyuo vya kutoa mafunzo ya u-DJ.