1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa mambo ya nje wa NATO wajadili msaada kwa Ukraine

3 Aprili 2024

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa 32 wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, wanakutana mjini Brussels leo, kujadili uungaji mkono wa Ukraine pamoja na mustakabali wa uhusiano wa jumuiya hiyo na Urusi.

https://p.dw.com/p/4eNVN
NATO Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa NATO Jens StoltenbergPicha: Saul Loeb/AP/picture alliance

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa 32 wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, wanakutana mjini Brussels leo, kujadili uungaji mkono wa Ukraine pamoja na mustakabali wa uhusiano wa jumuiya hiyo na Urusi.

Lengo la kikao hicho kilichopendekezwa na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenbergni kuhakikisha kwamba jumuiya hiyo si tegemezi kwa Marekani linapokuja suala la msaada kwa Ukraine.

Wanadiplomasia kadhaa wamedokeza kwamba kitita cha dola bilioni 108 kama msaada utakaotolewa kwa Ukraine katika kipindi cha miaka mitano ijayo, kitajadiliwa.

Sehemu ya pili ya mpango wa jumuiya hiyo kuongeza uungaji mkono wa muda mrefu kwa Ukraine inajumuisha, mpango mpya wa NATO wa kushirikisha uwasilishaji wa misaada ya kijeshi na mafunzo kwa jeshi la Ukraine.