1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbeki akutana na Mugabe na Arthur Mutambara wa chama kilichojitenga na MDC

5 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EWy8

HARARE

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini ambaye ni mpatanishi wa jumuiya ya nchi za maendelea za kusini mwa Afrika Sadc katika mgogoro wa Zimbabwe amekutana leo hii na rais Robert Mugabe mjini Harae kujaribu kuutatua mzozo wa kisiasa unaendelea nchini humo.Taarifa zinasema Mbeki na Mugabe wamefanya mazungumzo ya muda mfupi na baadae kuungana na kiongozi wa chama kidogo cha MDC kilichojitenga bwana Arhtur Mutambara pamoja na katibu mkuu wa chama hicho.Wakati huohuo kuemtolewa ushahidi mwingine unaofichua udanganyifu uliofanyika katika uchaguzi wa duru ya pili ya uchaguzi nchini Zimbabwe.Ushahidi huo ulirekodiwa kwa siri katika ukanda wa video na mlinzi mmoja wa gereza Shepherd Yuda ambaye ameshatoroka nchini Zimbabwe.Kwa mujibu wa taarifa zake Yuda ni kwamba watu walikuwa wakisimamiwa na kupewa amri wamchague rais Robert Mugabe.

Upinzani unadai kwamba makundi ya vijana wapiganaji wa rais Mugabe wamewauwa zaidi ya wafuasi wake 100 na kuwakamata wengine kiasi 1500 tangu mwezi Marchi.