Merkel na Sarkozy wataka ushirikiano wa karibu wa kiuchumi
17 Agosti 2011Matangazo
Katika kujaribu kuonesha mshikamano wao dhidi ya mgogoro wa madeni unaoikabili sasa sarafu ya Euro, viongozi hao wawili wametangaza pendekezo la kuwa na utunzaji sawa wa mahitaji ya bajeti kwa nchi hizo 17 zinazotumia sarafu ya Euro, katika katiba zao.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wao mjini Paris, kansela Merkel alisisitizia kwamba nchi zote wanachama wa eneo hilo la Euro zinapaswa kufanya kazi pamoja kuimarisha udhibiti wa uchumi.
Hata hivyo wawekezaji wameonekana kukatishwa tamaa na matokeo ya mkutano huo.
Kansela Merkel na Rais Sarkozy walikuwa katika shinikizo kufikia mipango ya kuunga mkono nchi hizo za Euro na kurejesha imani ya soko baada ya msukosuko uliodumu kwa mwaka mmoja na nusu.