1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili zaidi yaopolewa, na sasa watu 136 wathibitishwa kufa

John Juma
21 Septemba 2018

Kamishna mkuu wa jeshi la Polisi nchini Tanzania Simon Sirro amenukuliwa akisema kuwa miili ya watu 136 imeopolewa majini na wengine wengi hawajulikani waliko.

https://p.dw.com/p/35JTA
Tansania Fährunglück auf dem Victoriasee
Picha: DW/M. Magessa

Miili zaidi imeopolewa katika ziwa Victoria nchini Tanzania na kufanya idadi ya waliothibitishwa kufa kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere kuongezeka hadi 136.

Shughuli za uokozi bado zinaendelea, huku kukiwa na hofu huenda watu zaidi walikufa maji.

Waziri wa uchukuzi Isack Kamwele ameiambia televisheni ya taifa kuwa idadi hiyo ni ya kufikia leo mchana, na kuwa taarifa nyingine itatolewa jioni hii.

Kamishna mkuu wa jeshi la Polisi nchini Tanzania Simon Sirro amenukuliwa akisema kuwa miili ya watu 136 imeopolewa majini na wengine wengi hawajulikani waliko.

Ajali hiyo ilitokea jana. Watu 37 waliokolewa wakiwa hai.

Mkuu wa Wilaya Bw. Magembe azungumzia ajali ya MV Nyerere

Inahofiwa feri hiyo ilibeba watu wengi kuzidi kiwango kinachokubalika wakati mkasa huo ulipotokea.

Sudi Mnette amefanya mahojiano na mkuu wa wilaya ya ya Ukerewe Cornel Lucas Magembe aliyeko katika eneo la Busia ambako tukio hilo lilitokea na kwanza anazungumzia shughuzi za uokoaji. Sikiliza mahojiano hayo.

 

 

Mwandishi: John Juma

Mhariri: Lilian Mtono