1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mitandao ya kijamii na sheria ya uhalifu mitandaoni Tanzania

Mohammed Khelef
22 Novemba 2016

Ukuwaji wa matumizi ya mitandao ya kijamii miongoni mwa vijana nchini Tanzania unatajwa kuwa miongoni mwa sababu za serikali ya huko kuweka Sheria ya Kukabiliana na Uhalifu Mitandaoni mwishoni mwa mwaka 2015 ambayo tangu wakati huo imekuwa ikikosolewa kwa kuwaandama watumiaji wa kawaida wa mitandao hiyo wenye kutuma kauli zinazowakosoa viongozi na sio uhalifu hasa unaotendeka mitandaoni.

https://p.dw.com/p/2T2ui

Maxence Mello, ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao wa Jamii Forum, anapiga kampeni ya kufanyiwa marekebisho kwa sheria hiyo.