1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano maalum wa Umoja wa Mataifa juu ya malengo ya maendeleo ya Millenia.

Abdu Said Mtullya21 Septemba 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema malengo ya maendeleo ya Millenia yanaweza kufikiwa.

https://p.dw.com/p/PHs6
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: AP

NEW YORK:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameitaka jumuiya ya kimataifa iimarishe juhudi kwa ajili ya kufanikisha malengo ya maendeleo ya Millenia.

Akiwahutubia viongozi wa dunia kwenye mkutano maalumu wa kilele wa Umoja wa Mataifa, katibu Mkuu Ban alisema mjini New York kwamba licha ya viunzi vilivyopo njiani, malengo ya maendeleo ya Millenia yaliyopitishwa mnamo wa 2000 yanaweza kufikiwa.

Akizungumza kwenye kikao hicho maalum mjini New York, naye rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa alipendekeza hatua ya kuyaongezea kodi mabenki ili fedha zitakazopatikana zitolewe kwa ajili ya msaada wa maendeleo.

Viongozi na wakuu wa serikali zaidi ya mia moja wanaohudhuria kikao hicho maalumu cha siku tatu wanatathmini hatua iliyofikiwa hadi sasa katika kuyatekeleza malengo ya maendeleo ya Millenia.Malengo hayo ni pamoja na kupunguza kwa nusu kiwango cha umasikini duniani hadi utakapofika mwaka wa 2015.