1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa mataifa ya Amerika, huko Trinidad na Tobago

Nina Markgraf17 Aprili 2009

Swala la Cuba huenda likaibua tofauti kati ya Rais Barack Obama wa Marekani na nchi za Amerika.

https://p.dw.com/p/HZH5
Rais Barack Obama na Rais Felipe Calderon wa MexicoPicha: AP


Katika mkutano wa kanda hii unaoanza leo, huko Trinindad Tobago, vikwazo dhidi ya Cuba, na kutengwa kwa kisiwa hiki cha kikoministi, huenda ikatawala mkutano huo unaowaleta pamoja viongozi wa mataifa 33 ya Amerika. Cuba haihudhurii mkutano huo.


Obama na washirika wakuu wa Cuba, hasa rais wa Venezuela Hugo Chavez, wameshikilia misimamo tofauti kuhusiana na swala la Cuba hata kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa kilele, wa nchi za Amerika. Tayari ishara zinaashiria swala la Cuba, ambayo haihudhuri mkutano huu itatawala ajenda za mkutano huu.


Akiwa nchini Mexico, kabla ya kuelekea Trinidad Tobago, Rais Obama aligusia mvutano kati ya Cuba na Marekani hauwezi kusuluhishwa kwa usiku mmoja, kwani umekuwa kwa miaka karibu hamsini tangu yale mageuzi yaliyofanywa na Fidel Castro.


Chavez auf dem Balkon des Präsidentenpalastes in Caracas
Rais Hugo Chavez wa VenezuelaPicha: AP

Lakini Obama alisema hatua yake ya kuwaondolea vikwazo vya usafiri na kutuma fedha kisiwani Cuba, wamarekani walioa na asili ya Cuba ilikuwa ishara ya kutaka kufufua uhusiano wa mahasimu hawa wa Amerika, ingawa vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa Cuba miaka 47 bado vipo.

Rais Hugo Chavez katika mkutano na rais Raul Castro wa Cuba, Evo Morales wa Bolivia, rais wa Nicaragua, Honduras na Paraguay, viongozi wa ule muungano wa mrengo wa kushoto, aligusia kuwa atahakikisha swala la Cuba linatawala mkutano huu wa Amerika-


Raul Castro Präsident Kuba beim Besuch in Moskau Russland
RaIS Raul Castro wa CubaPicha: AP

Chavez ameonya kwamba nchi yake pamoja na mataifa mengine yatatumia kura zao za turufu kupinga taarifa ya mwisho ya mkutano huu kwa kuitenga Cuba.


Chavez amesema ana matumaini kwamba rais wa Marekani, Barack Obama, anahudhuria mkutano huo ili kuwasikiliza wakizungumza ukweli wa mambo na kwamba watataka kujua kwa nini Cuba haihudhurii mkutano huo.

Hakuna mpango wowote wa rais Obama kukutana ana kwa ana na rais wa Venezuela Hugo Chavez pembezoni mwa mkutano huo.


Castro amegusia kuwa nchi yake iko tayari kwa mazungumzo na Marekani kuhusiana na maswala ya haki za kibinadamu, uhuru wa vyombo vya habari, swala la wafungwa wa vita na maswala mengine yeyote. Lakini akaongeza watafanya hivi kwa sharti moja, iwapo Cuba itatazamwa kwa usawa


Katika kongamano la nchi za Amerika kusini, nchini Brazil mwaka jana Argentina, Brazil na Mexico zilitoa taarifa ya pamoja kuitaka Marekani iondoe vikwazo vya kiuchumi ilivyoviwekea Cuba.



Mwandishi: Munira Muhammad/afp

Mhariri: Abdulrahman