1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtambo wa mafuta wadhibitiwa na kundi la waasi

12 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CaSB

KHARTOUM:

Kundi la waasi wa Darfur JEM,limesema kuwa limeteka mtambo wa kuchimbua mafuta katika eneo la Kordofan,kati kati ya Sudan.Kamanda wa kundi hilo la waasi amesema,shambulizi hilo ni onyo kwa makampuni ya Kichina kuondoka Sudan.

Mtambo wa Rahaw unaoongozwa na kampuni ya Kichina,“Great Wall Company“ huzalisha hadi mapipa 35,000 ya mafuta kila siku moja na upo kaskazini-magharibi ya mtambo mwengine wa kuchimbua mafuta,ambao ulishambuliwa na kundi la JEM katika mwezi wa Oktoba.

Kundi hilo la waasi lilionya kuwa litalenga makampuni ya mafuta ya kigeni na hasa makampuni ya Kichina kwa sababu Beijing huiuzia silaha serikali ya Khartoum.