Mto Mara unaounganisha Kenya na Tanzania ni rasilmali inayotegemewa na wakazi wa nchi hizi mbili kwani unapitia kwenye mbuga ya Masai Mara hapa Kenya na ile ya Serengeti nchini Tanzania. Lakini mto huu unakumbwa na kitisho kikubwa kutokana shughuli za binadamu zinazotekelezwa karibu na hata vyanzo vya mto huo.