1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni aapa kuwaandama waliouwa watalii, muongozaji wageni

19 Oktoba 2023

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameapa kwamba vikosi vyake vya usalama vitawasaka waliohusika na mauaji ya muongozaji watalii na watalii wawili wa kigeni waliokuwa kwenye fungate katika mbuga ya taifa ya wanyama.

https://p.dw.com/p/4Xk3l
Uganda Yoweri Museveni Präsident
Rais Yoweri Museveni wa UgandaPicha: picture alliance/dpa/Russian Foreign Ministry

Maafisa wa Uganda wamelishtumu kundi la waasi wa ADF kuwauwa wanandoa hao, ambo walikuwa raia wa Afrika Kusini na Uingereza pamoja na muongozaji wao raia wa Uganda, Jumanne jioni katika Mbuga ya Wanyama ya Malkia Elizabeth II. 

Soma zaidi: Museveni alaani mauaji ya watalii

Kundi la ADF, ambalo lilianzisha uasi nchini Uganda na limekuwa likiendesha shughuli zake katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo tangu mwishoni mwa miaka ya 1990, lilitangaza utiifu kwa kundi la Dola la Kiislamu (IS) miaka minne iliyopita. 

Soma zaidi: Mauaji ya watalii yazusha wasiwasi Uganda

Kundi la IS limedai kupitia chanaeli yake ya Telegram kuhusika na shambulio hilo la Jumanne.