1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano wazidi kuitishia serikali ya Tshisekedi

Jean Noel Ba-Mweze9 Novemba 2020

Vyama vinavyomuunga mkono Rais mstaafu Joseph Kabila maarufu FCC, vimeionya CACH, muungano wake Rais Felix Tshisekedi, kuhusu jaribio lolote la kuvuruga bunge la taifa ili kujitafutia uwingi bungeni.

https://p.dw.com/p/3l3uS
Kongo Der kongolesischen Präsidenten Félix Tshisekedi zu Besuch am CHESD-College
Picha: Giscard Kusema/Pressebüro des Präsidenten

Katika taarifa iliyotangazwa baada ya mkutano wa kisiasa wa siku mbili, FCC imetaka kuandaliwe uchaguzi wa mapema kwenye ngazi zote, ili kuachia raia mamlaka ya kuamua. Tangazo hilo limekuja wakati rais Felix Tshisekedi akiendelea na mikutano yake ya mashauriano kwa lengo la kuunda umoja wa taifa. 

Mnamo Jumapili muungano FCC ulimaliza mkutano wake wa kisiasa na baada ya mkutano huo, muungano huo wake Joseph Kabila ukatangaza msimamo wake.

FCC inayoongoza nchi hii kwa ushirikiano na CACH, muungano wake rais Felix Tshisekedi imearifu pia kwamba ipo tayari kuzungumza naye rais Tshisekedi, ila yote yafanyike kufuatana na mpango wa mkataba waushirikiano. 

Baraza la seneti la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kenya
Baraza la seneti la Jamhuri ya Kidemokrasia ya KenyaPicha: AFP/Getty Images/J. D. Kannah

"FCC ina fuatilia kwa makini jinsi mikutano ya mashauriano iliyoanzishwa naye rais inavyoendeshwa, na inajulisha msimamo wake. Yaani, FCC ipo tayari kwamazungumzo naye rais ikiwa yatafanyika kama ilivyopangwa na mkataba wa ushirikiano." Ameeleza Nehemie Mwilanya, mratibu wa muungano FCC. 

Mambo mengine ambayo FCC imeyaonya ni pamoja na rushwa ambayo imedai inatolewa na muungano wake rais Tshisekedi kwa mabunge ili kukubali wajiunge na CACH, pia tishio la kulifuta bunge la taifa.

Aidha, FCC imesisitiza kwamba ipo njia moja tu ya kujipatia uwingi bungeni, nayo ni kupitia uchaguzi na ndiyo maana, muungano wake Joseph Kabila umesema upo tayari kwa uchaguzi wa mapema kwenye ngazi zote.

Vyama vinavyomuunga mkono Rais mstaafu Joseph Kabila maarufu FCC, vimeionya CACH, muungano wake Rais Felix Tshisekedi
Vyama vinavyomuunga mkono Rais mstaafu Joseph Kabila maarufu FCC, vimeionya CACH, muungano wake Rais Felix TshisekediPicha: REUTERS

Wito wa uchaguzi

Wito huo wa uchaguzi wa mambo ni jambo lisilokubalika upande wa Muungano wa Demokrasia na Maendeleo ya Jamii, UDPS, chama chake rais Felix Tshisekedi.

Kiongozi wa muungano wa vijana wa chama hicho, Ted Beleshay, ameieleza DW kwamba kutakuwa kwanza na mageuzi kabla ya uchaguzi.

"Sisi tunawaza kunapaswa kuwe na mageuzi katika tume ya uchaguzi, pia mageuzi ya sheria ya uchaguzi. Tunawo mda hadi mwaka 2023 kwa kufanya hayo, ili tuwe na tume itakayotoa matokeo yasiyo na mabishano. Kufuta bunge, mambo hayo yapo chini ya katiba kama alivyoeleza rais, ila kwa kweli hiyo ni hatua ya mwisho."

Wakati huu, Rais Felix Tshisekedi anaendelea na mikutano ya mashauriano kwa muda wa wiki moja sasa. Tukumbushe kwamba, ni FCC, yaani muungano wake Rais mstaafu Joseph Kabila ndio unao wingi wa viti bungeni.

Jean Noel Ba-Mweze, DW, Kinshasa.

Mhariri: Gakuba, Daniel