1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu Tanzania

Mohammed Khelef
23 Oktoba 2016

Sasa unatimia mwaka tangu Watanzania kumiminika vituoni kuchagua viongozi wao kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, na Maoni Mbele ya Meza ya Duara inauangazia mwaka huu mmoja na kile unachomaanisha kwa mpigakura wa kawaida: Je, kura yako imekuletea kile ulichokitazamia? Je, kipi kimebadilika kuwa vipi na kipi kingepaswa kuwa vipi? Vipi kuhusu suala la Zanzibar - limekwisha au bado lingalipo?

https://p.dw.com/p/2RZeG