1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Ongezeko la maambukizi ya HIV duniani

21 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqf

Repoti ya Umoja wa Mataifa inasema takriban watu milioni 4.3 duniani kote wameambukizwa upya na virusi vya HIV hapo mwaka 2006 na kuifanya idadi ya watu wanaoishi na viruri vya HIV kufikia karibu milioni 40.

Repoti hiyo imeelezea kuongezeka kwa idadi ya wahanga wa kike.Kikanda ongezeko kubwa kabisa katika viwango vya maambukizi limekuwa katika majimbo ya Urusi ya zamani,Kusini na Kusini Mashariki mwa Asia hususan kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya na ngono zembe.

Eneo la kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika bado linabeba mzigo wa janga hilo la UKIMWI ambapo karibu watu milioni 25 wameambukizwa sawa na theluthi mbili ya kila mtu mwenye kuishi na virusi vya HIV duniani.