1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Umoja wa Mataifa una wasiwasi kuhusu mapigano mapya Darfur

13 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQF

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kufuatia kuzuka upya mapigano katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Katibu mkuu wa umoja huo, Ban Ki Moon, ameliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mapigano mapya huko Darfur ambayo yamesababisha vifo vya raia 25.

Machafuko hayo yanajumulisha mashambulio ya mabomu ya angani ya yanayofanywa na jeshi la serijkali ya Sudan kulipiza kisasi mashambulio ya mwezi uliopita yaliyofanywa na kundi la waasi la Haki na Usawa, Justice and Equality Movement, dhidi ya kambi ya jeshi ya Wad Banda huko Haskanita.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tume ya Umoja wa Afrika nchini Sudan, mashambulio ya kinyama ya angani na ardhini katika eneo la Haskanita yalisababisha vifo hivyo vya raia 25.

Ban Ki Moon ametaka miito mipya itolewe kwa pande zinazohasimiana Darfur ziache mapigano ili kuwezesha mazungumzo ya kisiasa yafanyike mwezi Oktoba mwaka huu.