1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Washindi wa tunzo la amani la Nobel wataka biashara ya silaha idhibitiwe

24 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzf

Washindi 15 wa tunzo la amani la Nobel, wametoa mwito kwa nchi wanachama wa Umoja wa mataifa kuunga mkono mswada wa azimio la kudhibiti biashara ya silaha. Mswada huo wa sheria utapigiwa kura kesho katika mkutano mkuu wa Kamati ya Umoja wa mataifa inayohusika na swala la kupokonya silaha.

Mwito huo wa washindi wa tunzo la amani la Nobel, unaungwa mkono na mashirika kadhaa kama Shirika la udhibiti wa silaha ama Control Arms campaign, shirika la Oxfam na Shirika la kimataifa la udhibiti wa silaha ndogo ndogo, la IANSA. Miongoni mwa waliotoa mwito huo wa kudhibitiwa biashara ya silaha, ni pamoja na kasisi wa Afrika ya kusini, Desmond Tutu na kiongozi wa kidini wa watu wa eneo la Tibetan, Dalai Lama.

Nchi nyingi ikiwemo Ujerumani, zimesema zitaunga mkono azimio hilo.