1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nusu-finali kombe la Afrika

7 Februari 2008

Leo Ghana yaumana na simba wa nyika_kamerun wakati mabingwa Misri wana miadi na makamo-bingwa I.Coast.

https://p.dw.com/p/D40n

Katika kombe la Afrika la Mataifa leo ni leo na asemae kesho muongo:wenyeji Black Stars Ghana wakiania kuvaa taji lao la 5 la kombe la Afrika wana miadi na simba wa nyika-Kameroun mjini Accra kila mmoja akitapia taji lake la 5 .

Katika nusu-finali ya pili baadae usiku huu huko Kumasi,mabingwa Misri na makamo-bingwa Tembo wa Ivory Coast, wanakutana -mafiraouni wa Misri wakiwakumbusha Tembo wa core d’Iviore kuwa wembe uliowakata pembe zao katika finali ya 2006 mjini Cairo, ndio ule ule utakaowanyoa leo.Tembo lakini,wanadai „

Black Stars, wamewaahidi simba wa nyika kuwanasa kwa mtego ule ule waslioutumia kuwakamata Super eagles-mahasimu wao wa jadi –Nigeria.Ghana, mabingwa mara 4 wa kombe hili kati ya 1963 na 1982 wanadai hu uni mwaka wao ,lakini wanabidi leo kuteremka uwanjani hivi punde bila ya nahodha wao John Mensah,aliefungiwa kwa kucheza ngware na kutolewa nje ya chaki ya uwanja pale Ghana ilipifumania Nigeria kwa mabao 2-1.

Kwahivyo, jahazi bila ya nahodha mara nyingi huyumbayumba na hata kuzama.

Kocha mfaransa Claude Le Roy,anaemuangalia Mensah kama mlinzi bora kabisa wa kati ya uwanja ulimwenguni,anaungama kwamba bila ya Mensah hasa katika mechi na Kameroun ni tatizo kubwa.

Kamerun pia imetamba mara 4 katika Africa Cup tangu 1984 na baada ya kuteleza mbele ya mabingwa Misri ilipozabwa wa nyika wamerudi kun’guruma kwa kishindo.

Kocha wa simba wa nyika-mjerumani Otto Pfister amekuwa akigonga vichwa vya habari mjini Accra na baadhi si vya kupendeza: Baada ya kuonywa kutovuta sigara uwanjani kuwa huo ni mfano mbaya kwa chipukizi,jana alinyimwa ruhusa ya kuingia uwanjani na timu yake kwa mazowezi.Polisi wa Ghana walilikomea lango .Matokeo yake alirushiana ngumi na polis.Pfister,aliekosoa wazi wazi maandalaio ya kombe hili la Afrika,baadae alipita lango hilo na kuingia uwanjani kujiandaa kwa zahama ya leo na wenyeji Ghana.wiki iliopita,Otto Pfister alilalamika juu ya kuchelewa kwa ndege,kupotea kwa mizigo ya timu yake,hoteli kuwa si safi na kadhalika.Waghana leo kama wenyeji kwahivyo, wana kila sababu ya kumutia adabau Otto Pfister na simba wake wa nyika.Yeye,anapanga kuwapa adabu Black Stars.

Kama Ghana, Tembo wa Ivory Coast wanabidi kucheza bila ya beki wao mshahara, Kolo Toure wa ArsenalLondon.Toure alieumia alianza jana kujiunga tena kwa mazowezi na kikosi cha corte d’iviore.Iwapo atamudu leo kuteremka kuzima vishindo vya akiba abo trika wa Misri,ni swali la kusubiri kuona.

Katika changa moto hii ya pili ya kulipiza kisasi kwa tembo, macho zaidi yatakodolewa mikuki yao ya usoni kuhilikisha mahikalu ya mafiraouni: washambulizi 2 wa Chelsea-akina Didier Drogba na Salomon Kalou.

Misri pia inauguliwa na mshambulizi wake wa Bundesliga-ligi ya ujerumani-Mohamed Zidan na kuna shaka shaka iwapo Zidane alielifumania mara 2 lango la simba wa nyika-kamerun atamudu kucheza leo.Zidane hakucheza pale Misri ilipotoka suluhu bao 1:1 na chipolopolo-Zambia na wala hakuukanyaga uwanja Misri walipowafumania Angola kwa mabao 2:1.

Mazowezi ya jana ya Misri yalibidi kukatizwa kutokana na mvua ,waliweza lakini dakika 10 baadae kucheza.Na Zidane alishiriki katika mazowezi.