1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Tanzania yadai muuaji wa maafisa usalama ni gaidi

Daniel Gakuba
2 Septemba 2021

Polisi nchini Tanzania imesema kuwa mwanamme aliyewauwa kwa bunduki maafisa watatu wa polisi na mlinzi wa kampuni binafsi mwezi uliopita mjini Dar es Salaam alikuwa gaidi.

https://p.dw.com/p/3zpW9
 Inspector General Polizei  Tanzania IGP Simon Sirro
Picha: Police Communications Department

Mwanamme huyo aliyetambulishwa kama Hamza Mohammed, mnamo Agosti 25 aliwafyatulia risasi polisi wawili kwa kutumia bastola mjini Dar es Salaam, kisha akawapokonya bunduki zao na kuelekea kwenye ubalozi wa Ufaransa, ambako alimuuwa mlinzi.

kurugenzi wa Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Uhalifu nchini Tanzania (CID) Camilius Wambura, amesema uchunguzi wao umebainisha kuwa Hamza alikuwa gaidi.

Wambura amesema Hamza alikuwa akitazama mitandaoni ujumbe wenye misimamo mikali kutoka makundi ya kigaidi kama Al-Shabaab na lile linalojiita Dola la Kiislamu (IS).

Aidha, kulingana na maelezo ya mkuu huyo wa CID, mshambuliaji huyo alikuwa na mawasiliano na watu kutoka mataifa yenye vitendo vya kigaidi.