1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Port Moresby.Tetemeko la ardhi la chini ya bahari latokea huko Papua New Guinea.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1x

Kumetokea tetemeko kubwa la ardhi la chini ya bahari, kaskazini mwa Papua New Guinea.

Tetemeko hilo lenye ukumbwa wa 6.0 limetia khofu kuwa huenda ikawa ni dalili ya Tsunami katika nchi hiyo.

Hakuna taarifa zozote za hasara wala maafa yaliyotokana na tetemeko hilo.

Wakati huo huo umeme umerejea tena katika maeneo mengi ya kisiwa kikubwa cha Hawaii, baada ya kupotea kufuatia tetemeko kubwa la ardhi la siku ya Jumapili, lililopelekea kuharibika kwa mamia ya makaazi, njia na vitendea kazi vya bandarini.

Wafanyakazi bado wanaendelea kusafisha udongo na mapande ya ardhi yaliyoziba bara bara kuu iliyozunguuka kisiwa hicho.