1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Debby azungumzia Jamhuri ya Afrika ya Kati

MjahidA19 Aprili 2013

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati, ECCAS, inaendelea na mkutano wake nchini Chad wa kutafuta njia za mpito za kukabiliana na ghasia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati

https://p.dw.com/p/18JIs
Rais wa Chad Idriss Deby
Rais wa Chad Idriss DebyPicha: picture-alliance/dpa

Katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika mji mkuu wa Chad N'Djamena, Rais wa Chad Idriss Deby ambaye ni mweyekiti wa Jamii ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya kati ECCAS, amesema Jamhuri ya Afrika ya kati ni kama kidonda, kwa kuwa licha ya dawa zote ambazo imekuwa kikitiwa kidonda hicho, bado kimekataa kupona.

Rais Debby amesema ni lazima kuwe na mikakati ya kudumu ya kupambana na hali halisi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kuzuia machafuko na ghasia zaidi katika eneo hilo, baada ya mapinduzi yaliofanywa na waasi mwezi Machi 24.

Rais wa zamani Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize
Rais wa zamani Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois BozizePicha: dapd

Mwanzoni mwa mwezi huu ECCAS iliandaa mkutano mwengine kuzungumzia mapinduzi yaliofanywa na waasi yalioiondoa madarakani serikali ya nchi hiyo na kusababisha Rais Francois Bozize kuikimbia nchi yake.

Ghasia zaidi zashuhudiwa

Mwezi uliopita wanajeshi 13 wa Afrika Kusini waliuwawa mjini Bangui baada ya kushambuliana na waasi wa Seleka na mwishoni mwa wiki, takribani watu 20 waliuwawa baada ya mapigano kati ya waasi hao na raia wa mji huo wa Bangui.

Hata hivyo, waziri mkuu wa Jahmuri ya Afrika ya kati, Nicolas Tiangaye, aliviomba vikosi vya Ufaransa na pia usaidizi wa kijeshi kutoka katika mataifa jirani kusaidia kuimarisha usalama nchini humo.

Machafuko mjini Bangui
Machafuko mjini BanguiPicha: Reuters

Huku hayo yakijiri, Rais Debby amesema kikosi cha ECCAS kinachojumuisha wanajeshi 500 kutoka Gabon, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Chad hakiwezi kujitegemea katika kulinda amani katika jamhuri ya Afrika ya Kati.

Idadi ya wanajeshi wa kulinda amani vyaongezwa

Sasa viongozi wa jumuiya hiyo ya kiuchumi wamesema wataongeza wanajeshi takriban 2,000 ili kusaidia kurejesha amani udhabiti wa nchi hiyo. Suala la kuifadhili nchi hiyo baada ya kumalizika kwa mapinduzi pia ni kati ya mambo yaliyojadiliwa katika mkutano huo.

Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ambaye pia ni mkuu wa waasi wa Seleka, Michel Djotodia, anakabaliana na ukosefu wa fedha za kutosha katika maendeleo ya nchi hiyo.

Wanajeshi wa kulinda amani
Wanajeshi wa kulinda amaniPicha: SIA KAMBOU/AFP/Getty Images

Djotodia amesema wamechukua madaraka wakiwa na changamoto kubwa mno ya kukosekana fedha za kuendesha nchi.

Rais huyo wa mpito ameongeza kuwa waziri wake wa fedha kwa sasa anapata wakati mgumu sana kutafuta pesa za kuwalipa watumishi wa umma nchini humo.

Mwandishi: Amina Abubakar/dpa/AFP

Mhariri: Mohammed Khelef