1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Samia kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

George Njogopa23 Septemba 2021

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania atarajiwa kuhutubia kwa mara ya kwanza mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea jijini New York, Marekani.

https://p.dw.com/p/40j74
76. Generaldebatte der UN-Vollversammlung
Picha: Timothy A. Clary/AP/picture alliance

Hata hivyo nchini mwake kuna shauku kubwa ya kufuatilia hotuba hiyo atakayoitoa Alhamisi majira ya saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Ni hotuba inayotupiwa macho na wengi nchini Tanzania kwa kuwa itamtambulisha kwa mara ya kwanza Rais Samia katika hadhara hiyo kubwa kabisa kimataifa inayofanyika kila mwaka kwa viongozi wa nchi na serikali kujadili masuala ya kiulimwengu.

Wengi wanaamini hotuba yake itakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania na siyo tu kiuchumi bali pia kuboresha mahusiano ya kidiplomasia yaliyofifia kwa wakati fulani.

Akizungumza wakati alipowasili jijini New York, Rais Samia alisema Tanzania kama ilivyo nchi nyingine za dunia inapitia athari za kimazingira ingawa athari hizo pengine zisiwe kubwa kiasi hicho.
Akizungumza wakati alipowasili jijini New York, Rais Samia alisema Tanzania kama ilivyo nchi nyingine za dunia inapitia athari za kimazingira ingawa athari hizo pengine zisiwe kubwa kiasi hicho.Picha: DW/Said Khamis

Tanzania haijawahi kuhudhuria vikao hivyo kwa miaka mitano, wakati Rais wa awamu ya tano, hayati Rais John Magufuli alipomua kujishughulisha zaidi na masula ya ndani, huku majukuwaa mengi ya kimataifa akiwatuma wawakilishi wake.

Kuna uwezekano mkubwa Rais Samia katika hotuba yake akagusia maeneo kama vile athari zilizosababishwa na maambukizo ya virusi vya corona, haja ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kikanda na suala mtambuka la mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza wakati alipowasili jijini New York, Rais Samia alisema Tanzania kama ilivyo nchi nyingine za dunia inapitia athari za kimazingira ingawa athari hizo pengine zisiwe kubwa kiasi hicho.

Suala la uwekezaji na uimarishaji wa masoko ya ndani, ingawa pengine lisijitokeze sana kwenye totuba yake lakini ni mada iliyopewa uzito mkubwa katika ziara yake hiyo ambayo ni ya kwanza nchini Marekani akiwa ameabatana na ujumbe mkubwa wa wafanya biashara.

Rais Samia Suluhu alichukua usukani kufuatia kifo cha aliyekuwa mtangulizi wake John Magufuli
Rais Samia Suluhu alichukua usukani kufuatia kifo cha aliyekuwa mtangulizi wake John MagufuliPicha: AP/picture alliance

Innocent Shoo, mhadhiri wa chuo cha diplomasia cha jijini Dar es Salaam, anasema licha kwamba jukwaa la baraza kuu la Umoja wa Mataifa siyo mara zote linatumika kusaka maslahi ya kiuchumi, lakini jambo hilo linaweza kutiliwa maana pia katika ziara hiyo ya Rais Samia.

Rais Samia ambaye pia amekutana na jumuiya ya wafanyabiashara wa Marekani ameueleza pia Umoja wa Mataifa namna serikali yake ilivyoanza kuchukua hatua kuleta usawa wa kijinsia katika uongozi.

Hata hivyo, katika mitandao ya kijamii na rubaa za upinzani, wanaharakati wanakumbushia kwamba Rais Samia anahutubia hadhara hiyo kuu ya Umoja wa Mataifa, wakati shughuli halali za kisiasa za vyama zikiendelea kuzuiwa na vyombo vya dola na huku uhuru wa kidemokrasia ukiwa mashakani.