1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali nchini Kenya imezuia mali ya mtuhumiwa wa mauají ya halaiki nchini Ruanda Bw.Felicien Kabuga

7 Mei 2008

Serikali ya Kenya inazuia mali ya mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda Felicien Kabuga kwa lengo la kumzuia kukwepa kukamatwa au kuwasaidia watuhumiwa wengine kutoroka.

https://p.dw.com/p/Dvnh
Jumba la makumbusho ya mauaji ya halaiki nchini RwandaPicha: picture-alliance/ dpa

Hatua hiyo imetangazwa hapo jana jioni na Keriako Tobiko mkurugenzi wa mashtaka nchini Kenya.Felicien Kabuga ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa KiHutu anashtumiwa kufadhili wapiganaji walioshiriki katika mauaji ya halaiki ya mwaka 94 nchini Rwanda.Yapata watu laki nane walipoteza maisha yao katika vita hivyo vilivyodumu kwa siku 100.Mahakama ya uhalifu wa kivita kwa ajili ya Rwanda iliyoko mjini Arusha Tanzania inasikiliza kesi hiyo.

Kutoka Arusha Nikodemus Ikonko anaarifu zaidi