1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Depression Wissenschaft

Sekione Kitojo2 Desemba 2009

Sononeko ama mfadhaiko unajitokeza kuwa ugonjwa wa jamii, linasema shirika la afya ulimwenguni WHO.

https://p.dw.com/p/Kp9Q
Daktari akitoa ushauri kwa mgonjwa.Picha: dpa/pa

Kusononeka ama mfadhaiko unajitokeza kuwa ugonjwa wa jamii, linasema shirika la afya ulimwenguni WHO. Duniani kote kuna watu milioni 120 ambao wanasumbuliwa na maradhi hayo. Iwapo mtu hatapatiwa matibabu mara nyingi matokeo yake ni kujiua. Ripoti ya Volkhardt Wildermuth inazungumzia kuhusu ugonjwa huu, ambao kila mmoja wetu anaweza kuupata.

Nimekuwa nikupata mawazo yanayojirudia, hofu kuhusu maisha yangu, hofu kuhusu mtoto wangu. Kwangu mimi sifurahii tena maisha na baada ya hapo nikawa katika hali ya kutojijali tena, siwezi kula, na siwezi kulala.

Maisha ya mwanamke huyu yalitumbukia baadaye katika shimo refu lenye giza, na kufungiwa ndani. Uchunguzi ulionesha kuwa ni sononeko na mfadhaiko. Na sononeko la kweli ama mfadhaiko unatofauti kubwa na masikitiko ya kawaida, anasema daktari na mtaalamu wa ushauri wa magonjwa ya akili kutoka mjini Berlin Dr. Bernhard Palmosky.

Masikitiko katika hali ya juu kabisa inawezekana kuwa hisia kali za maumivu. Hii kila mtu anakumbana nayo, kama umepoteza ndugu ama iwapo kuna hali ya kutengana. Wakati huo huo hali ya hisia katika sononeko ina tabia ya kuwa na hisia za ombwe, na hisia za kuzungukwa na giza.

hali ya mambo ya kawaida inatoweka, nguvu zinapotea, na hakuna njia ya kutoka katika hali hiyo.

Ni ugonjwa mbaya sana, ambao mara kwa mara unadharauliwa, kwa sababu watu wanafikiri kuwa ni aina fulani ya kawaida ya sononeko tu, ambapo kila mmoja anafahamu , lakini ni ugonjwa mbaya sana ambao kwa bahati mbaya unaweza kumfikisha mtu katika hatua ya kujiua.

Sehemu kubwa ya watu wanaojiua hurudiwa na hali hii ya sononeko mara kwa mara , anaelezea mtaalamu wa masuala ya magonjwa ya akili Dr. Francesca Regen kutoka katika shirika la kutoa misaada. Idadi ya watu wanaojiua nchini Ujerumani imepungua kwa nusu tangu katika miaka ya 80. Hii inatokana na kwamba watu wenye mfadhaiko ama sononeko mara kwa mara hutafuta msaada wa kitaalamu.

Nafasi, kwamba kila mtu anaweza kuwa na afya nzuri ni nzuri sana, lakini inatofautiana kati ya mtu na mtu , tunaweza kusema kimsingi, ni ugonjwa mbaya sana, lakini unaweza kutibika.

Mtu awapo na hali mbaya ya kusononeka kuna matibabu dhidi ya sononeko na tiba ya magonjwa ya akili. Kwa hali ya kuanza taratibu , ni vizuri mtu kuwa na subira kwanza, mara nyingi hutokea hali kuwa mbaya katika muda wa wiki chache baadaye. Hali ya wastani ya sononeko inaweza kupatiwa msaada ikiwa katika aina yoyote ile, kwa vidonge ama hata kwa tiba ya ushauri wa waganga wa magonjwa ya akili ama kwa kutembelewa na marafiki. Kwa hiyo ni suala la uamuzi, kwamba suala gumu katika ugonjwa huu wa akili liko katika kuweza kuuondoa.

Francesca Regen anasisitiza, kuwa ugonjwa wa sononeko unaweza kumpata mtu yeyote.

Kuna hali ya tathmini ya kinasaba, ambacho hakiwezi pekee kuamua ama kwa mfano kuionyesha hali ya kuathirika kwa haraka , ili kuendeleza sononeko katika hali maalum. Kuna sababu pia za kibinafsi za kila mtu anavyojiweka, na pia maisha ya mtu binafsi, kwamba nimempoteza mtu muhimu wa karibu, nimepoteza kazi, na hapo vinakuja vichocheo vyote. Lakini kuna pia sononeko ambalo halina kichocheo.

Anasema Bernhard Palmowsky kuwa watu milioni nne nchini Ujerumani wanaugua ugonjwa huu wa sononeko. Duniani kote mara kwa mara kunapatikana ugunduzi wa ugonjwa huu. Shirika la afya la umoja wa mataifa WHO , linaeleza kwamba ifikapo mwaka 2020 ugonjwa wa sononeko utakuwa karibu na magonjwa ya moyo ukiwa ni ugonjwa wa pili mkubwa.

Mwandishi : Wildermuth, Volkhart/ ZR / Kitojo Sekione

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman.