1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Asili na mazingiraSudan Kusini

Shule za Sudan Kusini kufunguliwa tena

Tatu Karema
27 Machi 2024

Serikali ya Sudan Kusini, imesema shule nchini humo zitafunguliwa tena wiki ijayo baada ya kufungwa kwa wiki mbili kufuatia joto kali kote nchini humo.

https://p.dw.com/p/4eAZK
Bango hili linaonyesha onyo la joto kali katika eneo la Death Valley, nchini Marekani
Sudan Kusini inefungua tena shule zake baada ya kuzifunga kwa wiki mbili kutokana na joto kali. Maeneo mengi ulimwenguni hivi sasa yanakabiliwa na joto kali kutokana na mabadiliko ya tabianchiPicha: Bridget Bennett/REUTERS

Wizara za afya na elimu zimesema kuwa viwango vya joto vinatarajiwa kushuka kwa kasi huku msimu wa mvua ukitarajiwa kuanza katika siku zijazo.

Walimu wamehimizwa kupunguza shughuli za michezo ya nje na kuzifanya mapema asubuhi ama ndani ya madarasa, kuhakikisha hewa ya kutosha madarasani, kuwapa wanafunzi maji ya kunywa na kuwafuatilia wale watakaoonesha dalili za magonjwa yanayotokana na joto kali.

Waziri wa afya Yolanda Awel Deng amesema majimbo ya Bahr El- Ghazel, Warrap, Unity na Upper Nile ndiyo yalioathirika zaidi.

Masomo kwenye taasisi za juu na shule za maeneo ya mashambani ziliendelea na masomo licha ya tahadhari iliyotolewa na wizara ya elimu