1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sirte, Libya: Serekali ya Sudan inasitisha mapigano katika Mkoa wa Darfur

28 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7C1

Sudan imetangaza kwamba, kwa upande wake, inasitisha mapigano katika mkoa wa Darfur kusadifu wakati yanafanyika mazungumzo huko Libya yenye nia ya kumaliza michafuko iliodumu sasa miaka mine katika mkoa huo. Mshauri wa rais wa Sudan alitoa tangazo hilo mwanzoni mwa mazungumzo hayo yanayofanyika huko Sirte, Libya. Mwezi uliopita, rais Omar al-Bashir alisema yeye yuko tayari kuyasitisha mapigano kabla ya kufanyika mazungumzo hayo, Lakini mawili kati ya makundi ya waasi yameyasusia mazungumzo hayo kutokana na mzozo kuhusu makundi gani yawakilishwe mkutanoni, licha kwamba Umoja wa Mataifa umetishia kuyawekea vikwazo makundi yanayosusia. Mzozo wa Darfur umeanza mwaka 2003 na umechukuwa maisha ya watu laki mbili na zaidi ya milioni mbili kupoteza makaazi yao.