1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia: Rais atia saini sheria ya kurefusha muda wake

14 Aprili 2021

Rais wa Somalia ametia saini na kuwa sheria muswada wa kuendelea kusalia madarakani pamoja na serikali yake, wakati Marekani na mataifa mengine yakitishia kuiwekea vikwazo nchi hiyo iliyogubikwa na machafuko.

https://p.dw.com/p/3rz7l
Somalia Präsident Mohamed Abdullahi Mohamed
Picha: Vladimir Smirnov/TASS/imago images

Mvutano huo unaongeza mgogoro wa kisiasa wa miezi kadhaa baada ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari kucheleweshwa. Wakosoaji wanasema muda wa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed kusalia madarakani umemalizika.

Jamii ya kimataifa ilipinga sheria hiyo ya Rais Mohamed kuendelea kusalia madarakani, na imeonya kuwa kundi la kigaidi la Al-Shabab huenda likatumia mwanya huo wa mgawanyiko wa kisiasa kufanya mashambulizi.

soma zaidi: UN yawahimiza viongozi Somalia kuafikiana juu ya uchaguzi

Jana Jumanne, Rais huyo alitia saini sheria tata baada ya bunge nchini humo mapema wiki hii kupiga kura ya kuendelea kusalia madarakani kwa miaka miwili zaidi.

Hata hivyo, viongozi wa baraza la Seneti la nchi hiyo wamesema kura hiyo haramu.