1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan Kusini taifa jipya kabisa duniani

Martin,Prema/dpa9 Julai 2011

Sudan Kusini ni taifa jipya kabisa duniani kuanzia saa sita za usiku kuamkia leo Jumamosi na hivyo kujitenga na Sudan baada ya miongo kadhaa ya mapigano.

https://p.dw.com/p/RYp4
Am 9.7.2011 wird Südsudan ein unabhängiger Staat.
Sudan Kusini taifa huru jipya duniani

Kengele za kanisani zililia saa sita usiku, kuashiria siku hiyo ya kihistoria huku midundo ya ngoma ikilikaribisha taifa la 54 barani Afrika. Kuwepo kwa taifa hilo jipya, kutatangazwa rasmi leo asubuhi mjini Juba, katika sherehe zitakazofanywa, pale Rais Salva Kiir atakapoapishwa rais wa kwanza wa taifa hilo jipya.

Wakaazi katika mji mkuu Juba, walianza kusherehekea uhuru wa taifa lao tangu Ijumaa jioni kwa muziki na kupiga honi za magari mitaani.

Wiki ijayo Sudan Kusini inatazamiwa kupokewa kama nchi mwanachama wa 193 katika Umoja wa Mataifa.