1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan uchaguzi 2009

3 Agosti 2008
https://p.dw.com/p/EpkJ

Khartoum:

Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan ameahidi uchaguzi muhimu wa taifa uliopangwa mwaka ujao, kama sehemu ya utaratibu wa mageuzi ya kidemokrasi utafanyika kama ilivyopangwa.

Rais al-Bashir alikua akiwahutubia viongozi wa vyama vya wafanyakazi wa nchi za kiafrika na kiarabu waliokusanyika mjini Khartoum kulaani pendekezo la mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa, kutaka kiongozi huyo akamatwe kwa makosa ya mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na maovu dhidi ya binaadamu.

Wachambuzi wengi wanaashiri kwamba waranti uliotolewa na mahakama ya jinai ya kimataifa unaweza kuhujumu mkataba wa amani uliofikiwa kati ya kaskazini na kusini mwa Sudan 2005.

Al Bashir alitwaa madaraka katika mapinduzi ya kijeshi 1989 yalioiangusha serikali iliochaguliwa kidemokrasi.

Kwa mara ya kwanza kwa mujibu wa sheria mpya ya uchaguzi wa mwaka ujao, wanawake wametengewa asili mia 25 ya viti bungeni na kutakuweko na uakilishi kwa mujibu wa uwiano wa kura za vyama vya kisiasa.