1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania kuzipiga na Morocco katika mechi ya ufunguzi AFCON

17 Januari 2024

Mashabiki wa kandanda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki wanasubiri kwa shauku kubwa mechi kati ya Taifa Stars ya Tanzania na miamba wa soka Morocco katika michuano ya AFCON inayoendelea Ivory Coast.

https://p.dw.com/p/4bM4B
AFCON
Nembo ya Kombe la Mataifa ya Afrika Picha: Braima Darame/DW

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pia itaingia uwanjani baadaye leo kuchuana na Zambia katika mechi ya kundi F.

Wachezaji wa Taifa Stars wameonyesha imani ya kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Tanzania, Kongo kutupa karata ya kwanza michuano ya AFCON

Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndio timu pekee zinazoiwakilisha Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka huu katika michuano ya  Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON.

Jana usiku, Mali iliifunga Afrika Kusini 2-0 huku Tunisia ikiangukia pua mbele ya Namibia baada ya kupigwa 1-0.