1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Milipuko ya Mabomu jijini Dar Es Salaam

17 Februari 2011

Nchini Tanzania,idadi ya waliouawa baada ya milipuko kadhaa ya jana jioni kwenye ghala la silaha la jeshi la Gongo la Mboto imefikia kiasi ya watu 20.

https://p.dw.com/p/10IXT
Picha: dpa

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu aliyeliarifu bunge hii leo,watu wengine alfu 4 wanapata hifadhi katika uwanja wa kitaifa wa michezo.Duru zinaeleza kuwa maghala mengine 23 ya silaha,shule moja ya sekondari pamoja na nyumba mbili pia viliteketea kwenye mkasa huo.Itakumbukwa kuwa mlipuko wa aina hiyo uliwahi kutokea mwaka 2009 katika eneo la Mbagala.Ili kupata picha halisi Thelma Mwadzaya amezungumza na mwandishi wa Dar es salaam,George Njogopa aliyeutembelea uwanja wa kitaifa wa michezo.

Mtayarishaji:George Njogopa

Mpitiaji:Thelma Mwadzaya