1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yateketeza nyavu na zana haramu za uvuvi

Admin.WagnerD26 Januari 2017

Serikali ya Tanzania inafanya operesheni kabambe za kudhibiti uvuvi haramu pamoja na kukamata zana za uvuvi zisizotakiwa katika Ziwa Tanganyika.

https://p.dw.com/p/2WRxv
Tansania Kigomas Beauftragter Emanuel Maganga
Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu, Emanuel MagangaPicha: DW/P. Kwigize

Kitoweo cha samaki na dagaa licha ya kuwa muhimu katika ukanda wa maziwa makuu barani Afrika, uvuvi katika Ziwa Tanganyika nchini Tanzania unakabiriwa na changamoto nyingi ikiwemo urasimu wa upatikanaji wa leseni, uvuvi haramu na uelewa mdogo kuhusu shughuli za uvuvi.

Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kigoma imefanya operesheni ya kuteketeza nyavu zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 480 zilizokamatwa zilizokamatwa kaatika ziwa Tanganyika zikihusishwa na uvuvi haramu.

Akitekeleza zoezi hilo mkuu wa mkoa Meja jenerali mstaafu Emanuel Maganga amesema itapambana vikali na wavuvi haramu pamoja na waigizaji, wauzaji na watumiaji wa zana zisizoruhusiwa katika uvuvi.

Wakati huo huo serikali ya Tanzania imekanusha kuwepo kwa Uvuvi unaotumia sumu katika ziwa Tanganyika. Hivi karibuni zilisambaa taarifa kuwa katika ziwa hilo lonalotoa huduma za uvuvi katika nchi za Tanzania, Burundi na DRC kwamba sumu hutumika kuua samaki.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Meja Generali mstaafu Emmanuel Maganga ametoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari akikanusha na kufafanua kwamba samaki waliokutwa wameharibika hawakuuwawa na sumu.

Meja Jenerali maganga ameeleza kuwa kilichobainika baàda ya uchunguzi ni samaki wanaoharibika ni wanaonaswa na nyavu katika kina cha chini na kuchelewa kuvuliwa hasa nyakati za usiku ambapo maji ya ziwa huwa ya moto.

Tansania getrocknete jleine Fische
Dagaa katika Mwalo wa samaki na dagaa wa Kibirizi mjini KigomaPicha: DW/P. Kwigize

Afisa Uvuvi mkoa wa Kigoma Bi. Ritha Mlinga ameonya kuwa wavuvi wote wanaoweka mitego au nyavu na kuziacha ziwani kwa muda mrefu wanapaswa kuacha Tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo ndio wanaosababisha kuoza kwa samaki walionaswa na mitego yao

Tansania  Fischfang-Vertretterin Ritha Mlinga und Rechercher Dr. Shimael Kimerei
Bi. Ritha Mlinga, afisa Uvuvi Mkoa wa Kigoma (kushoto) na Azizi Daudi, afisa uvuvi manispaa ya Kigoma UjijiPicha: DW/P. Kwigize

Wakati huo huo mtafiti mkuu wa masuala ya Uvuvi Tanzania anayesimamia tafiti katika ziwa Tanganyika Dr. Ishimael Kimerei ametahadharisha kuwa endapo shughuli za uvuvi katika ziwa hilo hazitazingatia sheria ipo hatari ya kutoweka kwa aina mbalimbali ya samaki ikiwemo Migebuka na Dagaa ambazo zinatajwa kuwa na thamani katika soko la dunia.

Tansania  Moskito-Netze
Vyandarua vya mbu vilivyokamatwa vikitumika kuvua dagaa ziwaniPicha: DW/P. Kwigize

Aidha Imebainika kuwa baadhi ya wavuvi wa samaki na dagaa katika ziwa Tanganyika wanatumia vyandarua vya kujikinga na mbu waenezao Malaria ambavyo baadhi yake vina sumu jambo ambalo ni la hatari kwa afya za watumiaji wa maji na rasilimali za ziwa Tanganyika.

Mwandishi: Prosper Kwigize

Mhariri: Josephat Charo