1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Umoja wa Mataifa hauna msimamo mmoja asema Ahmedinejad

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtS

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran amekosoa vikali azma ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kutaka kuiwekea Iran vikwazo kwa sababu ya mradi wake wa kinuklia ulio na utata.Ahmedinejad, amelituhumu baraza hilo kuwa halina msimamo mmoja.Alipozungumza hii leo,alisema nchi zinazomiliki silaha za kinuklia zinawazuia wengine haki ya kutumia teknolojia ya kinuklia kwa matumizi ya amani.Ametamka hayo siku moja baada ya rais wa Urussi Vladimir Putin kukutana na Ali Larijani mjini Moscow.Larijani,ni mpatanishi mkuu wa Iran katika majadiliano yanayohusika na mradi wa kinuklia wa Iran.Teheran inasisitiza kuwa inataka kuzalisha nishati na inapinga kabisa madai ya Marekani kuwa inajaribu kutengeneza silaha za kinuklia.