1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

The HAGUE:Katanga mbele ya mahakama ya kimataifa

23 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7DW

Mbabe wa kivita ,Germain Katanga anaetuhumiwa kutenda uhalifu wa kivita kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo amefikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya mjini the Hague kwa mara ya kwanza tokea akamatwe.

Katanga anakabiliwa na madai ya kutenda uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita. Anatuhumiwa kuhusika na shambulio la mwaka 2003 lililofanywa na waasi katika jimbo la Ituri ambapo raia 200 waliuawa.

Mtuhumiwa Katanga alikamatwa miaka miwili baada ya tukio hilo na alifikishwa kwenye mahakama ya kimataifa ya mjini the Hague nchini Uholanzi wiki jana.