1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi na Kabila wazungumzia mageuzi ya tume ya uchaguzi

Saleh Mwanamilongo
13 Machi 2020

Rais Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila wametathmini makubaliano yao ya kugawana madaraka,kufuatia kuibuka kwa tofauti nyingi baina yao.

https://p.dw.com/p/3ZNzg
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi (R) na mtangulizi wake Joseph Kabila siku ya kupeana madaraka mjini Kinshasa.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi (R) na mtangulizi wake Joseph Kabila siku ya kupeana madaraka mjini Kinshasa.Picha: picture-alliance/AP Photo/J. Delay

Tshisekedi akutana na Kabila - MP3-Stereo

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila wamekutana mjini Kinshasa ambako walitathmini makubaliano yao ya kugawana madaraka, kufuatia kuibuka kwa tofauti nyingi baina yao. Wiki za hivi karibuni hali ya kutoaminia ilijitokeza baina ya maafisa wa serikali na idara za kiuslama kutoka vuguvugu la FCC la Kabila na lile la CACH la rais Tshisekedi.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mazungumzo baina ya viongozi hao iliyosomwa hii leo na Vital Kamerhe kiongozi wa ofisi ya rais Felix Tshisekedi, inaelezea kuwa mazungumzo baina ya Tshisekedi na Kabila yalifanyika katika hali ya utulivu. Kamarhe amesema miongoni mwa masuala waliozungumzia ni pamoja na mageuzi ya mfumo wa uchaguzi na pia tume ya uchaguzi.

''Viongozi hao wawili wameamua kuepo na mazungumzo ya mara kwa mara kwa ajili ya mwenendo bora wa mkataba wao wa uongozi wa pamoja,na wamekubaliana kuanzisha mazungumzo kwa ajili ya mageuzi ya mfumo wa uchaguzi nchini''ilielezea taaifa ya pamoja.

Tshisekedi awekewa shiniko ilikupambana na rushwa

Raia waliohuzuria shere za kuapishwa kwa rais Tshisekedi mjini KInshasa
Raia waliohuzuria shere za kuapishwa kwa rais Tshisekedi mjini KInshasaPicha: picture-alliance/AP Photo/J. Delay

Mkutano huo baina ya Kabila na Tshisekedi umekuja baada ya vita vya maneno baina ya wafuasi wa vyama vyao . Kila upande umelaumu mwingine kwa kutokuwa na nia nzuri katika utekelezwaji wa mkataba wa ushirikiano.

Vuguvugu la FCC la Joseph  Kabila ambalo linao wingi wa viti bungeni, kwenye baraza la seneti limesema kwamba rais Tshisekedi na wafuasi wake wamekuwa wakiwandama baadhi ya maafisa wa zamani wa serikali. Huku wafuasi wa Tshisekedi wakielezea kwamba mawaziri kutoka chama cha Kabila hawawajibiki vyema katika kazi yao.

Kisa cha hivi karibuni cha kutoaminiana baina ya washirika hao wawili ni kifo cha jenerali Delphin Kahimbi ambae alikuwa naibu mkuu wa jeshi na mtu wa karibu wa rais wa zamani Joseph kabila ambae alikutwa amefariki nyumbani kwake siku moja baada ya kuachishwa kazi na rais Tshisekedi.

Lubunga B'ya Ombe, mshauri wa aliekuwa rais wa Kongo Joseph kabila amesema kwamba ni hatua nzuri viongozi hao wawili kukutana licha ya kwamba hali bado niya kutoaminiana.

''Kukutana kwao ni kitu kizuri licha ya kwamba hali bado niya kutatanisha,lakini kwa vile waligusia masuala muhimu ambayo ni kuangalia uwezekano wa mageuzi ya tume ya uchaguzi'' alisema Lubunga.

''Lakini pia waligusia ugavi wa madaraka kwenye makampuni ya umma, hapo naweza kusema kwamba ni hatua nzuri ukilinganisha na hali ilivyo kuwa siku chache zilizopita''aliendelea kusema.

Siku za hivi karibuni,rais Felix Tshisekedi amewekewa shinikizo na mashirika ya kiraia, kanisa katoliki na baadhi ya nchi za magharibi ili kuchukuwa hatua kali katika kupambana na rushwa na uongozi mbaya.