1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi mkuu nchini Africa Kusini

21 Aprili 2009

Chama tawala ANC chatarajiwa kushinda kwa kishindo

https://p.dw.com/p/HbW9
Kiongozi wa chama cha ANC Jacob ZumaPicha: AP

Wakati wananchi wa Africa Kusini wakisubiri kwa hamu kubwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu hapo kesho,mgombea wa chama tawala cha National Congress Party ANC Jacob Zuma amepuuzilia mbali matamshi yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa upinzani juu ya kutilia shaka uadilifu wake hasa linapokuja suala la kukabiliana na rushwa. Jacob Zuma kiongozi wa chama tawala cha African National Congress Party ANC anatarajiwa kwa kiasi kikubwa kupata ushindi katika uchaguzi mkuu wa kesho. Kura za maoni zinaonyesha kwamba ANC kitajipatia asilimia 60 ya kura zote za uchaguzi huo na kumuweka Zuma katika nafasi nzuri ya kuchaguliwa rais mpya wa nchi hiyo wakati bunge litakapokutana mapema mwezi wa Mei. Zuma amesema anaaimani kwamba chama chake kitaungwa mkono na waafrica kusini wengi huku akipuuzilia mbali shakashaka za upinzani kuhusiana na suala la uadilifu wake baada ya kukabiliwa na mashataka ya rushwa ambayo yalitupiliwa mbali wiki mbili zilizopita.Akizungumza hii leo mbele ya waaandishi wa habari Zuma alisema-

Tunatazamia idadi kubwa ya wapiga kura katika uchaguzi wa kesho na tunatarajia kwamba watu wa nchi hii kwa mara nyingine watakiingiza madarakani chama cha ANC kwa wingi mkubwa,tufanye kazi kwa pamoja tuimarishe maisha yao''

Südafrika Wahl Parteien ANC
mmoja wa wafuasi wa ANCPicha: AP

Katika kampeini yake amezungumzia sana kuanzisha harakati za kubalina na rushwa licha ya kwamba binafsi alihusishwa na kashfa kadhaa za rushwa zilizotupiliwa mbali baadae.Tume huru ya uchaguzi nchini humo IEC imesema kwamba inatarajia wapiga kura watajitokeza kwa wingi.Tayari zaidi ya watu millioni 20 wanatazamiwa kupiga kura katika vituo 19,726 vya kupigia kura kote nchini ambavyo vitafunguliwa kuanzia saa moja asubuhi.

Juu ya hayo lakini kumekuwa na wasiwasi uliojitokeza juu ya uongozi bora ikiwa Zuma ataingia madarakani mtu ambaye anakumbatiwa na jamii ya waliomaskini lakini asiyeaminika mbele ya macho ya watu wa tabaka la kati kwasababu hadi yake iliyoingia dosari na hofu juu ya kuwaegemea zaidi washirika wake katika chama cha ANC wa mrengo wa kushoto.

Zuma mwenye umri wa miaka 67 mwanaharakati wa zamani aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi na ambaye pia alifungwa jela kwa muda wa muongo mmoja pamoja na mzee Nelson Mandela amekuwa akipigia upatu katika kampeini zake suala la kukabiliana na rushwa pamoja na utawala bora.

Rais wa sasa Kgalema Motlante aliyechukua nafasi hiyo baada ya kutimuliwa madarakani Thabo Mbeki mwezi septemba amesisitiza kwa upande wake amesisitiza kwamba Demokrasia nchini Africa Kusini bado ni madhubuti licha ya wimbi la kashfa serikalini.

Kwa upande mwingine wingi wa thuluthi mbili bungeni ambao umekuwa ukikipa uwezo chama cha ANC kuibadili katiba wakati wowote ni suala ambalo linakabiliwa na changamoto kutoka kundi jipya lililojitenga na chama hicho la Congress of The People COPE lililoundwa kufuatia mgawanyiko baada ya Thabo Mbeki kutimuliwa.Kama alivyoweka wazi mgombea wa urais wa chama hicho askofu wa zamani Mwune Dandala-

''Sisi,tutailinda katiba kwa kuhakikisha kwamba tuna taasisi zitakazohakikisha waafrika kusini wote wanazingatia katiba,raia wote watakuwa sawa mbele ya sheria''

Chama cha COPE ni miongoni mwa vyama 40 vinavvyoshiriki uchaguzi,vyama 26 vikiwa katika ngazi ya kitaifa na 14 mikoani.Wakati wachambuzi wa mambo wakisema ANC huenda kikapoteza wingi wake kutokana na chama cha COPE Zuma anasisitiza kwamba chama hicho hakitobadili chochote.

Mwandishi-Saumu Mwasimba

Mhariri Mohd Abdul-Rahman