1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchunguzi huru: Hakuna ushahidi wa chuki dhidi ya Uyahudi DW

8 Februari 2022

Wataalamu waliochunguza madai kwamba baadhi ya wafanyakazi wa DW walichapisha maudhui ya chuki dhidi ya Wayahudi mtandaoni, wamesema hawakupata ushahidi wowote kuthibitisha madai hayo.

https://p.dw.com/p/46hQ0
Screenshot PK Deutsche Welle Antisemitismusbericht
Picha: Deutsche Welle/dpa/picture alliance

Timu ya wataalamu huru iliwasilisha matokeo ya uchunguzi wake siku ya Jumatatu, kufuatia ripoti katika vyombo vya habari nchini Ujerumani, kuhusu chuki dhidi ya Wayahudi na matamshi ya chuki dhidi ya Israel yaliodaiwa kufanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Deutsche Welle (DW), ambalo ni shirika la utangazaji la kimataifa Ujerumani.

Uchunguzi huo ulitathimini matamshi ya wafanyakazi wa DW yaliowekwa kwenye akaunti zao binafsi za mitandao ya kijamii, pamoja na matamshi yaliochapishwa na viombo vya nje.

Soma pia: Waandamana Berlin kupinga chuki dhidi ya Uyahudi

Uchunguzi huo pia uliwahusisha washirika wa utangazaji wa DW katika kanda za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (Kanda ya MENA), kufuatia ripoti za vyombo vya habari nchini Ujerumani zilizobainisha maudhui ya chuki dhidi ya Wayahudi, katika machapisho ya vituo hivyo washirika wa DW.

DW-Antisemitismusbericht Screenshot des Livestreams
Mkurugenzi Mkuu wa DW Peter Limbourg.Picha: DW

Uchunguzi ulihitimisha kwamba hakukuwa na ushahidi kwa DW katika masuala ya chuki dhdi ya Wayahudi, lakini hatua lazima ichukuliwe kwa kutoa mafunzo.

Mkurugenzi mkuu wa DW  Peter Limbourg kutokana na matokeo ya uchunguzi, wafanyakazi watano watafanyakazi tena na DW

"Leo tumekubali makosa yetu na hayatajiruda,tutayashughulikia haya kikamilifu,tutatoa matokeo ya wazi pamoja na yale yaliohusiana na wafanyakazi" alisema Limbourg.

Kilichogunduliwa kwenye uchunguzi

Uchunguzi huo huru ulifanywa na timu ya wataalamu iliojumuisha mwanasaikolojia na mtaalamu wa kupinga chuki dhidi ya Uyahudi Ahmad Mansour na waziri wa zamani wa sheria Ujerumani Sabine Leutheusser-Schnarrenberger.

Soma pia: Dunia yaadhimisha mauaji ya halaiki ya Holocaust

Kufuatia mahojiano na wafanyakazi wa idhaa ya kiarabu ya DW pamoja na utafiti wao wenyewe, wataalamu hao walihitimisha kwamba, masuala yalioripotiwa na vyombo vya habari vya Ujerumani, yalikuwa ni matukio ya kibinafsi ambayo hayakuhusisha idara ya uhariri.

"Chuki ya kitaasisi dhidi ya Uyahudi haikuonekana," Mansour ambae ni mwanzilishi wa mpangio wa kukuza democraisa na kuzuia itikadi kali, alisema kwenye mkutano na  waandishi wa habari.

DW-Panel „Jüdisches Leben in Deutschland"
Mkuu wa DW Peter Limbourg akizungumza kwenye kamati ya Wayahudi nchini Ujerumani.Picha: JAN ROEHL/DW

Hata hivyo, wataalamu hao walibainisha kwamba maoni ya wafanyakazi watano wa DW yalionesha wazi chuki dhidi ya Wayahudi, kukanusha mauaji ya Holocaust, pamoja na matamshi yanayopinga haki ya kuwepo kwa Waisrael. Kusimamishwa kwa mwanzo kwa wafanyakazi hao kulikuwa "sahihi."

"Matamshi hayo yaliowekwa kwenye akaunti binafsi za mitandao ya kijamii, lakini yakiwa ya wazi," alisema Leutheusser-Schnarrenberger.

Wataalamu hao waliongeza, kazi ya uhariri iliofanywa na idhaa ya kiarabu ya DW iligundulika kuwa haina chuki dhidi ya Uyahudi,lakini visa vya kibinafsi vilivyogunduliwa viaweza kuharibu sifa ya DW.

Mansour na Leutheusser-Schnarrenberge waliotoa wito wa kuwepo kwa utaratibu wa bora wa kuajiri, kadhalika kufanya mafunzo kwa wafanyakazi wa DW waliopo, kuhusu chuki dhidi ya Wayahudi, Israel na mtzozo wa Mashariki ya Kati.

Soma pia: Miaka 75 tangu kambi ya Auschwitz ilipokombolewa

Ripoti hiyo pia ilipendekeza kufanyike marekebisho Idhaa ya Kiarabu ya DW na kuwe na "mwanzo mpya" ili kuleta mabadiliko.

Kuhusu ushirikiano wa  DW mashirika ya utangazaji ya ndani katika Kanda ya MENA, wameshauri kuwe na ushirikiano zaidi na mashirika mawili ya utangazaji, wamehimiza mazungumzo na miongozo ya wazi juu ya chuki dhidi ya Wayahudi na wengine.

Tayari DW ilikuwa imesitisha ushirikiano na shirika la utangazaji la Jordan,Roya TV, baada ya kugundua kuwa kituo hicho kilikuwa kikieneza maoni na katuni za kuchochea chuki dhidi ya Wayahudi.

Diplom-Psychologe Ahmad Mansour und NRW-Antisemitismusbeauftragte Sabine Leutheusser-Schnarrenberger
Wachunguzi wa madai ya chuki dhidi ya Wayahudi ndani ya DW, Ahmad Mansour na Sabine Leutheusser-Schnarrenberger. Picha: DW

Hatua zipi zilichukuliwa na DW?

Mkurugenzi mkuu Limbourg alisema DW itafanya mabadiliko makubwa kama matokeo ya uchunguzi huo huru

" Mimi pamoja na Menejimenti tunaomba radhi kwa dhati. Mashaka tu ya uwepo wa chuki dhidi ya Uyahudi katika taasisi inayofadhiliwa na fedha za walipa kodi wa Ujerumani, ni suala lisilovumilika kwa jamii ya Wayahudi nchini humu na kote duniani," alisema.

Limbourg aliongeza: " Lazima tuweke msimamo wetu wazi katika siku zijazo. Uhuru wa kujieleza kamwe hauwezi kuhalalisha chuki dhidi ya Wayahudi, kuichukia Israel na kukanusha mauaji ya Holocaust."

Karl Jüsten, mkuu wa baraza la utangazaji la DW alisisitiza kuwa DW inasera isiovumilia kabisa chuki dhidi ya Wayahudi na aliwashukuru Mansour na Leutheusser-Schnarrenberger, kwa tathmini yao.

Soma pia: Viongozi duniani wakemea kuongezeka kwa chuki dhidi ya Wayahudi

"Wameisaidia DW katika hali ngumu na wameunda msingi wa maboresho thabiti kutokana na uchunguzi wao" alisema Jüsten.

Mkuu wa Idhaa ya Kiarabu ya DW amewajibika kwa kujizulu kutoka nafasi yake na DW tayari imekubali hatua hiyo, alisema Limbourg. Mchakato wa kumtafuta mkuu mpya unaendelea.

DW pia itaainisha tafsiri ya wazi ya chuki dhidi ya Uyahudi kwa wafanyakazi wote, pamoja na kuimarisha sera ya maadili ya kazi, mchakato wa mafunzo na sheria za uajiri.

Deutsche Welle Logo
DW ni shirika la utangazaji wa kimataifa la Ujerumani.Picha: YURI KADOBNOV/AFP

Wito wa utekelezaji wa haraka

Rais wa baraza kuu la Wayahudi Josef Schuster, ameitolea wito DW kuchukua hatua za haraka na za wazi kutekeleza mabadiliko yalioanishwa kwenye ripoti hiyo.

"Shirika hilo linapaswa kutekeleza kwa haraka mapendekezo ya wataalamu," alisema. "Katika kipindi cha robo mwaka,  Deutsche Welle inapaswa kuwasilisha ripoti ya awali inayotoa taarifa juu ya hatua zilizochukuliwa."

Soma pia: Mipaka ya uhuru wa maoni inamalizikia wapi ?

Claudia Roth, Kamishna wa utamaduni na vyombo vya habari wa serikali ya Ujerumani, alibainisha kuwa DW ina wajibu mahsusi ambao inapaswa kuusimamia kama shirika la utangazaji la kimataifa la Ujerumani.

 "Katika matangazo yake, DW inapaswa kuheshimu na kulinda heshima ya utu. Hivyo ndivyo inavyosema sheria ya DW," alisema Roth katika taarifa. Alisema wajibu huo unawahusu wafanyakazi wote wa DW.

Roth, ambae ni mjumbe wa baraza la utangazaji la DW, ameutolewa wito uongozi wa DW kupendekeza orodha ya hatua stahiki, zikiwemo hatua za kimuundo, ambazo zitajumuisha idara za uhariri na utawala katika shirika hilo.

DW, shirika la utangazaji la  kimataifa la Ujerumani linalofadhiliwa kwa pesa ya walipa kodi, linatoa habari katika lugha 32 kwa mataifa kote duniani.

Chanzo:DW