1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yasema majeshi ya mataifa hayana nia ya kumuuwa Gaddafi

4 Mei 2011

Ufaransa imesema majeshi ya umoja wa mataifa yapo katika jitihada za kupunguza nguvu za kijeshi za Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kwa kushambulia vituo vyake vya kijeshi na wala si kumuuwa.

https://p.dw.com/p/118hm
Ndege ya kivita ya Ufaransa ikiwa katika opereshini nchini Libya
Ndege ya kivita ya Ufaransa ikiwa katika opereshini nchini LibyaPicha: AP

Akizungumza na kituo cha televisheni cha France 24, cha huko Ufaransa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wa nchi hiyo, Alain Jupe amesema lengo kubwa si kumuuwa Gaddafi.

Jupe, alikuwa akizungumzia tukio la hivi karibuni ambapo mashambulizi ya NATO yalisababisha kifo cha mmoja kati ya watoto wa kiongozi huyo mjini Tripoli.

Katika mahojiano hayo, alisisitiza kuwa walilenga maeneo ya kijeshi mjini humo, kunyong'onyesha nguvu za kijeshi za Gaddafi dhidi ya waasi ambao wanatambuliwa na Ufaransa. na kuonfgeza kwamba nchini harakati hizo, zinakwenda sambamba na jitihada za kisiasa katika kutafuta suluhu.

Aidha alisisitza kwamba wataendelea na mashambulizi ya anga dhidi ya majeshi ya Gaddafi mpaka wahakikishe wameumaliza kabisa uwezo wa kijeshi wa kiongozi huyo.

Jupe amekataa mapendekezo ya kusitisha mapigano yaliyotolewa na Gaddafi akidai kufanya hivyo kunaweza kusababisha kugawanyika kwa nchi katika pande mbili za mashariki na magharibi. Hata hivyo alisisitiza kwamba kiongozi huyo aondoe majeshi yake katika miji waliyovamia.

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa
Rais Nicolas Sarkozy wa UfaransaPicha: AP

Awali Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkoz alisema Ufaransa imepanga mdahalo wa wazi wa "marafiki wa Libya" kujadili mabadiliko ya mpito ya kisiasa nchini humo.

Wakati huo huo jeshi la Libya leo limevurumisha makombora ya roketi katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Zintan huko eneo la nyanda za juu za maashariki za nchi hiyo na umoja wa Mataifa unaesema vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo imesababisha maelfu kuikimbia nchi hiyo kwa miguu na wengine kwa boti.

Upande wa waasi umesema mizizimo zaidi za 40 ya makombora ya roketi imefyatuliwa mji wa Zintan huku misaada ya kiutu ikiwasilishwa katika bandari ya magharibi ya Misrata ambao pia imegubigwa na maashambulizi ya mizinga.

Libyen Misrata Rebellen
Miripuko imetokea nchini LibyaPicha: AP

Mjini Tripoli nako, mambo si shwari, mashuhuda wamesema mapema leo imesikika miripuko miwili ingawa hakukuwa na ufafanuzi kiini cha chake.

Gaddafi, ambae ameingia madarakani katika mapinduzi ya 1969, hajaonekana hadhariani tangu kufanyika kwa Mashambulizi ya NATO ya jumamosi ambayo yamemuuwa mtoto wake wa mwisho na wajukuu wake watatu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya, ´Khaled Kaim amesema kiongozi huyo yupo hai na mwenye afya njema na hajajeruhiwa hata kidogo na makombora ya NATO.

Kaem amesema leo atakutana na viongozi wa kikabila na kwamba suala la Gaddafi kuonekana hadharani litategemea hali ya usalama kwa kuwa amenusurika kwa zaidi ya mara nne sasa.

Mwandishi: Sudi Mnette/RTR/AFP

Mhariri: Abdul-Rahman